Jumatatu, 4 Aprili 2016

Vyakula Bora Anavyostahili Kula Mama Anayenyonyesha



Chakula bora ni muhimu sana kwa mama anayenyonyesha, kwanza kwaajili ya kuimarisha afya yake mwenyewe na pili kwaajili ya uzarishaji wa maziwa yenye virutubisho sahihi kwaajili ya mtoto.

Ifuatayo ni orodha ya vyakula 8 bora anavyostahili kula mama anayenyonyesha;

1. Blueberries
Blueberries
Matunda madogo aina ya BLUEBERRIES (Zabibu) yana virutubisho na madini muhimu kwajiri ya afya bora ya mama anayenyonyesha.

2. Maziwa
maziwa
Maziwa yana virutubisho vya kutosha aina ya Calcium, ambavyo ni muhimu kwaajili ya afya ya mifua ya mtoto.

3. Machungwa
machungwa
Moja ya virutubisho muhimu kabisa kwa afya ya mama anayenyonyesha ni virutubisho vya vitamini C, ambavyo vinapatikana kwa wingi katika machungwa.

4. Maji
maji-ya-kunywa
Maji ni sehemu kubwa na muhimu sana kwatika mwili wa mwanadamu kwaajili ya kuratibisha shughuli mbalimbali za kimwili, ikiwemo ya uratibishaji wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

5. Samaki
samaki-aina-ya-salmon
Samaki mfano wa Salmon na wengine wana virutubisho aina ya Docosahexaenoic acid (DHA) kwa wingi, ambavyo ni muhimu kwaajili ya afya ya mfumo wa neva za fahamu (Nervous System) za mtoto. 

6. Mayai
mayai
Mayai yana virutubisho vya Protini kwa wingi, ambavyo ni muhimu kwaajili ya kujenga afya ya mama anaye nyonyesha na mtoto.

7. Mboga za Majani
mboga-za-majani
Mboga za majani hasa zile za kijani ni muhimu sana kwa afya ya mama anayenyonyesha na mtoto kwakuwa zina virutubisho vya Vitamin A kwa wingi, ambavyo ni muhimu kwaajili ya afya ya macho na kinga ya mwili.

8. Maharage
maharage
Maharage yana kemikali aina ya Amino Acid, ambayo huungana kutengeneza Protini ambayo ni muhimu kwaajili ya ujenzi wa mwili.

0 comments: