Tabora New Hope Agency

Is aiming to improve the standard of living of the people in a community by planning on the utilization of the available resources and guiding on the implementation of the plans to achieve the best social services in Tanzania.

Tabora New Hope Agency

Is aiming to improve the standard of living of the people in a community by planning on the utilization of the available resources and guiding on the implementation of the plans to achieve the best social services in Tanzania.

Tabora New Hope Agency

Is aiming to improve the standard of living of the people in a community by planning on the utilization of the available resources and guiding on the implementation of the plans to achieve the best social services in Tanzania.

Tabora New Hope Agency

Is aiming to improve the standard of living of the people in a community by planning on the utilization of the available resources and guiding on the implementation of the plans to achieve the best social services Tanzania.

Tabora New Hope Agency

Is aiming to improve the standard of living of the people in a community by planning on the utilization of the available resources and guiding on the implementation of the plans to achieve the best social services Tanzania.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HADITHI/VISA NA MIKASA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HADITHI/VISA NA MIKASA. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 5 Agosti 2016

Ushuhuda: Nilimlisha Mume Wa Mtu Limbwata La Nyama Ya Bundi.

USHUHUDA  WA   THEOFLIDA  WA  YESU : NILIMLISHA  MUME  WA  MTU, LIMBWATA  LA  NYAMA  YA  BUNDI.

Nawasalimu  wa  jina  la  YESU,  jina  kuu  kupita  majina  yote. Jina  langu  ninaitwa  Theoflida , ni mwanamke  mwenye  umri wa  miaka  38  mkaazi  wa    Mbezi  ya  Kimara  jijini  Dar  Es  Salaam, japo kiasili  ni  mwenyeji  wa  wilaya  ya  Ulanga, mkoani  Morogoro..

Nime amua  kuandika  waraka  huu  kwa  madhumuni  makuu  mawili, kwanza  ni  kushuhudia  MATENDO  MAKUU  ambayo  YESU  AMENITENDEA  na  pili, ni  kuwa  hasa  wanawake  wenzangu  kutojihusisha  kabisa  na   masuala  ya  WAGANGA  WA  KIENYEJI  kwa  sababu  waganga  wa  kienyeji ni  MAWAKALA  WA  KAZI  ZA  SHETANI  HAPA  DUNIANI  na   ni  MASHETANI  KABISA!...

Nitaanza  kwa  kuelezea  kisa  kilicho  nipelekea  kuingia  kichwa  kichwa  kwenye  mikono  ya  wakala  wa  shetani..

Nilikuwa  nimepanga  chumba  kimoja  maeneo  ya  Tabata  Mawenzi  huku  nikijihusisha  na  biashara  ya  genge.  Jirani  na  nyumba  niliyokuwa  nimepanga, aliishi   mwanaume  mmoja  na  mke  wake. Mwanaume  huyu  jina  lake  linaanzia  na  herufi  K  hivyo  katika  maelezo  yangu  nitakuwa  nikimtaja  kwa  herufi  K.

K  alikuwa  ni  mwanaume  mwenye  mafanikio  makubwa  katika  maisha  mwenye  kazi  nzuri.   Alikuwa  na 

Jumamosi, 12 Machi 2016

SIMULIZI FUPI.

SIMULIZI FUPI: ULAANIWE
MTUNZI: George Iron Mosenya
TAHADHARI: Simulizi hii ni ya kubuni na haina uhusiano na maisha halisi ya mtu yeyote.
**************************

Kabla sijakuandikia haya nilivuta kumbukumbu ya miaka kadhaa nyuma Maria. Siku ile tulipokutana kisimani kuteka maji, macho yetu yakatazamana na sote kwa pamoja tukajikuta tukiona aibu.
Haikuwa mara ya kwanza kuonana lakini ile ilikuwa siku maalumu, ukaniomba nikutwishe ndoo ya maji, wakati nainyanyua tukatazamana tena machoni na kujikuta tukitabasamu. Haikuwa mara ya kwanza kutabasamu, lakini hii siku ilikuwa ya aina yake.

Siku ambayo nafsi zetu zilishindwa kutunza siri na kwa pamoja zikakiri kuwa zilikuwa zinahitajiana. Nilikwambia nakupenda nawe ukajibu unanipenda pia.
Maisha yetu duni hayakutuzuia kufurahi, nyumbani kwetu tukipika magimbi nilijitahidi kuficha pande moja na kukuletea shuleni, na wewe ulinihifadhia mahindi ya kuchemsha na kuniletea katika kile kisima tulichokutana mara ya kwanza.
Nakumbuka hekima zako na jicho lililoona mbali, ulisema tusishiriki ngono kwani mwalimu wa sayansi alidai kuwa ni hatari kwa afya na pia husababisha mimba kabla ya wakati.
Nilikusifu na kisha nikateta na moyo wangu nikisema wewe ni msichana wa kipekee sana kwangu. Msichana mwenye ndoto za maisha.

Darasa la saba likamalizika, sikubahatika kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kama ilivyokuwa kwako. Ulilia pamoja nami na almanusura ugome kwenda shule uliyochaguliwa, nikakusihi usome ili siku moja tuiendeshe familia yetu vyema, na hapo rasmi nikajikita katika kilimo.
Maria ukaenda shule huku ukisisitiza kuwa unanipenda sana,

Jumatano, 9 Machi 2016

SIMULIZI FUPI: MWISHO WANGU

MWISHO WANGU
SIMULIZI FUPI
Mwandishi: Iam Frank

TAHADHARI: Kisa hiki ni chakubuni hakina uhusiano na maisha halisi ya mtu yeyote!!!!!!
*******************************
 
Nilidhani kubadilisha ndoto zangu na kuvurugikiwa ilihitaji miaka mingi jambo hilo kutokea. Nilidhani kuisha kwa uzuri wangu na kila nilichokianzisha toka nilipokuwa mdogo ilihitajika miaka mingi kama ile niliyokuwa nayo sasa. Nilikuwa msichana mdogo sana na mwenye ndoto kubwa ambazo tayari sasa zilikuwa zimetimia. Kuwa na magari ya kifahari na familia yenye furaha ndicho kitu nilichokiwaza katika muda wote wa maisha yangu. Hatima ya maisha yetu anayeijua ni mungu na kamwe huwezi kumuona na kumuomba muda zaidi maisha yafikapo tamati, kila kitu huvurugika pale jioni ya maisha yako ifikapo. Milango ya ndoto zako hufungwa na giza nene hutanda mbele, fimbo ya kukuongoza njia hupotea. Mwanga hufifia na woga hukusonga. Hiyo ndiyo hali iliyonipata, machozi na jasho vikanitoka, aliyekuwa awe msaada wangu akanikimbia na kunisahau. Hata wale niliowadharau mwanzoni na kuwaona hawawezi kuwa chochote kwangu wala kunipa msaada nilitamani sasa wajitokeze lakini haikuwa hivyo.
Msichana mrembo nikageuka kuwa kituko mbele ya jamii, maringo yangu yote na elimu yangu havikunisaidia kupata huruma ya wanajamii.