KWA mara ya kwanza kongamano la diaspora
limefanyika Pemba. Ni kongamano la tano kufanyika nchini. Katika
kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 18, mwaka huu
katika Viwanja vya Kufurahishia Watoto vya ZSSF Tibirinzi, Wilaya ya
Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.
Kupitia hotuba yake, Dk Shein amewataka Diaspora kutambua kuwa wana jukumu lililo sawa la kuijenga Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa nafasi na uwezo walionao, ikiwa kwa kiuchumi au kielimu. Zaidi, Dk Shein aliwataka wanadiaspora wasiwe miongoni mwa kundi la wachache wanaodharau nchi zao kwa maendeleo yaliyofikiwa na nchi nyengine.
“Maendeleo ya kweli hayaji kwa kutupiana lawama na hayaji kwa misingi ya utashi, bali maendeleo ya kweli yanahitaji bidii na maarifa katika utekelezaji wa majukumu yao, umoja na mshikamano pamoja na matumizi mazuri ya rasilimali zilizopo,” alisema Dk Shein. Aidha, aliwakumbusha wanadiaspora umuhimu wa kutumia na kuweka akiba na huku wakikumbuka kusaidia nyumbani. “Msile mkamaliza, mle mkisaza,” alishauri.
Aliweka bayana pia, kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekamilisha Sera ya Diaspora ambayo ilizinduliwa rasmi Mei 9, mwaka huu kwa lengo la kuhakikisha mipango ya maendeleo. Pamoja na mambo mengine, Dk Shein alieleza kuwa Sera inaeleza na kufafanua mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwashirikisha Wanadiaspora katika fursa za kijamii na kiuchumi zilizopo kwa Wanadiaspora na namna bora ya kuzitumia fursa hizo.
Dk Shein alitumia fursa hiyo kuiagiza Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari Wanaoishi Nchi za Nje iliopo katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuhakikisha kwamba kopi ya Sera hiyo inawekwa katika Tovuti ya Idara kwa haraka iwezekanavyo ili Wanadiaspora wengi zaidi wapate kuisoma.
Aidha, Dk Shein alisema kuwa hivi sasa suala la kuwashirikisha Wanadiaspora katika kuimarisha maendeleo ya nchi zao za asili limepewa umhimu wa pekee na nchi mbali mbali duniani pamoja na Ushirikiano ya Kimataifa. Alieleza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kuandaa mikakati mbalimbali ya kuwashirikisha Wanadiaspora katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo, ambapo Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2010-2015 ilianza kuweka mikakati maalum juu ya ushiriki wa Wanadisapora katika kuijenga nchi yao.
Sambamba na hayo, Rais Dk Shein aliwahakikishia Wanadiaspora kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawakaribisha kwenda kuwekeza Zanzibar na kuwahakikishia kuwa suala la ardhi wasiwe na wasiwasi kwani wahusika wapo akiwemo Waziri anayeshughulikia ardhi Zanzibar, Salama Aboud Talib na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nassor.
Pia, Dk Shein aliwasihi Wanadiaspora kuendelea kuwa Mabalozi wazuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi wanazoishi na kuendelea kuwa mfano wa tabia njema ili kuendeleza sifa ya ukarimu, urafiki na usalama ambayo raia wa Tanzania wamejijengea na inatambulika katika mataifa yote duniani. Dk Shein aliwataka wanadiaspora kuendeleza kwa ari na kasi utamaduni wa kuja kutembelea nyumbani kila baada ya muda jambo ambalo ni muhimu na linaimarisha mapenzi.
Kwa ujumla wake kongamano lilifana sana kwa waandaaji kuandaa programu iliyoingiza vionjo mbalimbali ilikiwamo ngoma za utamaduni kutoka Unguja na Pemba. Na kwa kufanikiwa huko, hakika hizi ni jitihada za kupongezwa zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwakutanisha wanadiaspora. Hii ni fursa pia ya walio nje kuziona fursa za kiuchumi ndani ya Zanzibar. Itakumbukwa, Rais wa Zanzibar, Dk Shein alipata kutamka: “ Zanzibar inajiuza kwa jina lake.”
Ni kauli yenye kutoa tafsiri ya Wazanzibar wenyewe, walio Visiwani na Diaspora, kuanza kuyaangalia yale yenye tija kwa Wazanzibar wakianzia na hata jina linalobeba utambulisho wa visiwa hivyo. Kwa upande wa washiriki, kama ilivyokuwa katika makongamano manne yaliyotangulia, wameonesha kufurahia kuzitambua fursa za kiuwekezaji zilizopo Zanzibar. Ni Ukweli pia kuwa Zanzibar ni mahali pazuri sana kufanyia mikutano ikiwamo makongamano kama haya.
Zanzibar ingeweza kabisa kuwekeza pia kwenye utalii wa mikutano. Kwamba ivutie wale wenye kupanga kufanya mikutano midogo na mikubwa waifanyie Zanzibar. Zanzibar ina fukwe nzuri. Kufanyia mikutano mahali kama Zanzibar kunawavutia pia washiriki. Isitoshe, katikati ya mkutano, ni rahisi kupanga ziara za kitalii za umbali mfupi kama vile kutembelea mashamba ya viungo.

0 comments:
Chapisha Maoni