Jumapili, 13 Machi 2016

MANDE/MTUNGO (GANG RAPE)

KUPIGA MANDE/MTUNGO NI HATARI


Bila shaka neno ' Mande ' sio geni katika jamii zetu.
Mande inatokea pale kikundi cha watu wa jinsia ya kiume kinapomuingilia kimwili mtu mmoja kwa zamu.
Kitendo hiki cha wanaume zaidi ya mmoja kumuingilia mtu mmoja, wengine huita 'Mtungo' Kitendo hiki ni ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.

Mpaka watu kuamua kupiga mande inachangiwa zaidi na vijana kukosa shughuli maalumu ya kufanya na kukaa kwenye makundi ambayo yanawaingiza kwenye Misukumo Rika na kushawishiana kufanya vitendo vya uwovu.

Watu wengine hupiga mande kwa makusudi ya kumkomoa msichana ambaye amekuwa anakataa
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wavulana.

Aidha wapo ambao hufanya vitendo hivyo kwa kukodiwa ili kumkomesha Msichana/Mwanamke kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuwa na mahusiano na Mume/Bwana wa Msichana/Mwanamke mwingine.

  • Watafiti wamegundua kuwa wahalifu na waathirika wa matukio haya wengi wao ni vijana.
  • Wengi wanaojihusisha na mambo haya huwa ni wale wanaotumia pombe na madawa ya kulevya.
  • Wakati mwingine silaha hutumika kumjeruhi mtendewa ili lengo la watendaji liweze kutimia.
Mande humuacha muathirika katika hali mbaya na wakati mwingine hata kufa.

WANAUME WAWAJIBIKE KWASABABU:
Wanaume ndio wanaohusika zaidi na ishu hizi za kupiga mande, Unabishaaa?
Umeshawahi kusikia mwanamume amepigwa mande na wanawake? sio kitu cha kawaida kwa wanawake kupiga mande!!!!

  • Wanaume mtambue kuwa kitendo hiki ni cha hatari.
  • Kiini cha mabadiliko ni mwanaume.
  • Ni vizuri pale tunapoona kuwa kuna dalili ya vijana kujiingiza katika vitendo viovu tuwe msatari wa mbele kuhamasisha mabadiliko Chanya.
  •  Mwanaume atambue haki na wajibu wake na utii wa sheria za nchi.
  • kupiga mande ni ubakaji.
WANAWAKE PIA WAJIBIKENI:

Ni vema wanawake/wasichana kuepuka tabia zenye kuchochea kutokea kwa vitendo hivyo.

  • Jiepushe na tabia mbaya za kuwa na mahusiano na waume/mabwana wa watu.
  • Jiepushe na tabia za kupenda zawadi na ofa za starehe kutoka kwa mwanaume ambaye huna mpango wa kuwa nae kwenye mahusiano kwa sababu siku akijua kua unamzingua inaweza kuwa hatari kwako.
  • Achana na tabia ya kuwa kwenye mahusiano na mwanaume zaidi ya mmoja!!! hiyo ni hatari sana!!!
KUMBUKA:
  • Mande husababisha madhara mengi yakiwemo kupata maambukizi ya magonjwa ya ngono na hata VVU.
  • Mande ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
  • Kupiga mande ni Uvunjaji wa sheria za nchi na kwa mujibu wa sheria za Tanzania, adhabu kali ikiwemo kifungo mpaka cha maisha jela, faini kubwa, viboko n.k hutolewa kwa waliopiga mtungo na hata walioshiriki kupanga na kufanikisaha tendo hilo ovu.
Kila mtu awe na utashi na utii wa sheria.
**************************

0 comments: