Watu wengi wamekuwa wakifikiri kwamba upweke ni kuwa wao peke yao. Na hivyo ili kuondokana na upweke wamekuwa wakikazana kuhakikisha wanazungukwa na watu wengi.
Licha ya kuzungukwa na watu hao wengi bado upweke walionao hauishi. Bado wanajiona wapweke licha ya kuwa kwenye kundi kubwa la watu.
Badala ya kutatua tatizo la upweke ambalo watu wanalo, wamekuwa wakitafuta njia za kukimbia tatizo hilo, kulificha lisionekane. Na wamekuwa wakificha tatizo hilo kwa kutaka kuzungukwa na watu wengi na kuepuka kuwa peke yao. Na dunia hii ya sasa ambapo mitandao ya kijamii inatuunganisha na
dunia kwa masaa 24 kwa siku, njia za kukimbia upweke zimekuwa nyingi zaidi.
dunia kwa masaa 24 kwa siku, njia za kukimbia upweke zimekuwa nyingi zaidi.
Kwa uwepo wa mitandao hii hata mtu anapopata nafasi ya kuwa yeye mwenyewe, haraka sana
anaingia kwenye mitandao ili kujua kipi kinaendelea huko. Hii yote inazidi kukuza tatizo hili na inaweza kufika wakati likashindikana kufichika na madhara yakawa makubwa.
anaingia kwenye mitandao ili kujua kipi kinaendelea huko. Hii yote inazidi kukuza tatizo hili na inaweza kufika wakati likashindikana kufichika na madhara yakawa makubwa.
Dawa ya upweke, Ni kujikubali wewe mwenyewe kwanza. Kama huwezi kujikubali wewe mwenyewe, kwa vile ulivyo, hata uzungukwe na watu wengi kiasi gani, hata uwe kwenye mitandao gani ya kijamii, bado
utajisikia mpweke. Bado utaona kuna kitu hakijakamilika kwako na utaona maisha yako yana kasoro.
Na ili kujikubali ni lazima ujijue wewe mwenyewe, na utajijua kwa kupata muda tulivu wa kuwa wewe
mwenyewe, kuyatafakari maisha yako na kujua kipi unapendelea na kipi unaweza vizuri.
Pale unapoweza kukaa wewe mwenyewe na usijione mpweke, hapo ndipo unapokuwa umetibu tatizo la upweke. Usikimbilie watu au mitandao ya kijamii, anza na wewe mwenyewe.

Ukweli ni kwamba upweke hautokani na wewe kukosa watu kwenye maisha yako, bali unaanzia ndani yako mwenyewe, kwa kutokujijua vizuri na kujikubali. Dawa ya upweke ni kujijua vizuri na kujikubali kwa vile nilivyo. Usikimbilie tena kuzungukwa na watu au mitandao ya kijamii kuondoa upweke wako, badala yake anza kuondoa upweke ndani yako.
UJUMBE WA LEO.
The time you feel lonely is the time you most need to be by yourself. - Douglas Coupland
The time you feel lonely is the time you most need to be by yourself. - Douglas Coupland
(Wakati unapojisikia upweke ndio wakati unahitaji kuwa peke yako).
Dawa ya upweke sio kuzungukwa na watu au kuingia kwenye mitandao ya kijamii, bali kujijua na kujikubali vile ulivyo.
0 comments:
Chapisha Maoni