Alhamisi, 24 Machi 2016

HOFU YAKO, ADUI YAKO




Pamoja na hofu zote ulizokuwa nazo siku za nyuma kuhusu siku za sasa, nyingi hazijatokea. Na hata kama zimetokea mambo hayakuwa mabaya kama ulivyokuwa unafikiria. Nina hakika na hili kwa sababu bado upo na bado unaendelea kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Inawezekana Umekuwa ukihofia ya kwamba mambo yatakwenda vibaya, na kuanguka sana kwa kile ambacho unafanya, lakini baadae unakuja kugundua kuwa sehemu kubwa ya hofu zako hazijatokea.
Mara nyingi hofu ya kile kitakachotokea baadae huwa ni matokeo ya ubongo wako kujaribu kuweka hali ya utetezi juu ya kile ambacho unatamani kukichukulia hatua. Wakati wote unapojaribu kutaka kufanya kitu ambacho hujawahi kukifanya kabla, au kupitia njia ambayo hujawahi kuipitia kabla lazima sehemu Fulani ya nafsi yako itakupa maonyo ambayo mara zote huambatana na mifano na picha za kufikirika kuhusu hatari iliyoko mbele yako.

Wakati mwingine ubongo wako unaweza kukutengenezea mifano  na kukuletea picha za kuogofya kuhusu matukio kadhaa ya hatari yanayoweza kutokea hapo baadae ikiwa tu utaamua kuchukua hatua au njia unayotaka kuifuata.  

Lakini ukweli ni kwamba hiyo ni hofu tu na hofu hutengenezwa na fikra zako ili kukupa sababu za kujitetea ili usiamue kuchukua hatua muhimu kwenye maisha yako.

JARIBIO DOGO;
Jaribu kukumbuka mara zote ambazo umekumbana na houfu juu ya jambo ambalo ulitaka kulifanya (na labda ulilifanya)…..

Yaandike yote kwa mpangilio…..

Kasha fanya tathmini Je;
1.       Ni mambo mangapi ambayo hukuyafanya kutokana na hofu iliyoinuka juu yake?
2.       Ni mambo mangapi ambayo uliyafanya baada ya kuzidharau hofu zilizoinuka juu yake?
3.       Je ni mambo mangapi ambayo uliyafu kuwa yangetokea na yakatokea kweli?

Ninaamini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya vitu ulivyowahi kivihofia kuwa vingetokea HAVIKUTOKEA!!!
Kama hivyo ndivyo basi hii inamaana kuwa Vitu vingi unavyohofia leo kuhusu kesho yako,kuna uwezekano mkubwa kwamba  havitatokea, japo kwa sasa unaweza kuwa unaogopa sana, lakini nina hakika asilimia 90 ya unavyoogopa sasa wala havitatokea.
  • ·         Hivyo acha kuitumia hofu kama sababu ya wewe kuacha kuchukua hatua, kwa sababu sehemu kubwa ya hofu zako hazitatokea.
  • ·         Badala ya kuitumia hofu kama kikwazo, itumie hofu kama taarifa, kama tahadhari kwamba kuna uwezekano wa mambo kwenda tofauti na unavyotegemea. Na kwa kuwa na taarifa hizi utaweza kujiandaa vyema ili usifikie kwenye hali mbaya.
  • ·         Usikubali hofu ikuzuie kufanya makubwa, bali itumie kama kichocheo cha wewe kwenda mbali zaidi.

Ukweli ni kwamba pamoja na hofu nyingi ambazo umekuwa nazo, nyingi hazijawahi kutokea
na hata zilizotokea mambo hayakuwa mabaya kama ulivyokuwa unategemea.
Kuanzia sasa amua kutokurudishwa nyuma na hofu, itumie hofu kama kichocheo kwako kufanya
kwa ubora zaidi.

CHUKUA HII.
“Fear is not real. The only place that fear can exist is in our thoughts of the future. It is a product of our imagination, causing us to fear things that do not at present and may not ever exist. ― Will Smith.

Hofu siyo kitu halisi. Sehemu pekee ambapo hofu ipo ni kwenye mawazo yetu ya siku zijazo. Ni zao la taaswira tunayojijengea, inayotufanya tuhofie vitu ambavyo havipo sasa na huenda visiwepo kabisa.

Usikubali hofu ikuzuie, bali itumie kama kichocheo. HOFU YAKO NI ADUI YAKO!!!

0 comments: