Mahali popote ulipo umezungukwa na fursa kibao. Kama hujaziona
tatizo sio kwamba fursa hazipo tatizo ni macho yako hayazioni ila zipo. Katika makala
hii tutajifunza namna ya kuboresha macho yako na akili yako ili upate nguvu ya
kuziona fursa mahali ulipo.
Katika chapisho lililopita tuliangazia kuhusu uwepo wa fursa kwenye maeneo mbali mbali, sasa hebu tujaribu kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kuziona fursa hizo mahali tulipo.
Hizi hapa ni mbinu nne zinazoweza kukusaidia kuona fursa zinazokuzunguuka hapo ulipo;

Mbinu
ya kwanza: Kuwa Makini (Be Aware).
Kama huzioni fursa mpaka sasa unatakiwa kuanzia leo uanze
kutazama kwa macho ya kuona fursa.
Ili uweze kuziona fursa anza kuwa makini, chochote unachokiona chukua dakika chache kukitafakari huku ukijiuliza hii ni fursa? Ukikuta kuna watu wanalalamikia jambo fulani wewe tafakari hii ni fursa? Kama kuna rafiki yako anakwambia kuna jambo la kufanya sehemu fulani wewe tafakari hii ni fursa?. Unapotembea barabarani unakutana na watu wanasema vitu vimepanda bei au vimeshuka bei wewe tafakari hii ni fursa?. Unapangiwa ajira mkoa ambao hukuwa na mategemeo ya kufika huko wakati mwingine ule mkoa hauna mazingira uliyokuwa unayahitaji, usilaumu wewe jiulize hii ni fursa? Kuwa makini namna hii kunakufanya uweze kuziona fursa nyingi ambazo watu wengine hawazioni.

ya pili: Kila Unachokiona Kiite Fursa.
Mbinu hii ya pili ni nzuri sana itakusaidia kuziona fursa nyingi. Licha ya kuwa makini, kwenye mbinu hii ya pili,kila unachokiona usikione kama kilivyo kione kama fursa yako. Mfano, umehamishwa kiofisi ukapelekwa eneo lingine badala ya kujiuliza uliza uliza unatakiwa ujiambie na ujisemee huko ninapopelekwa ni fursa kubwa.
Usisikilize maneno ya watu wewe jisemee tu “lazima kutakuwa na fursa nyingi” na kweli ukifika anza kuona kila kitu unachokutana nacho kama fursa. Kwa njia hiyo utaona fursa nyingi sana.

ya tatu: Soma Vitabu Ili Uone Fursa Nyingine. Kuwa mpenzi wa
kusoma vitabu vingi. Kutoka kwenye vitabu utagundua kuna fursa nyingi sana. .
Mbinu
ya nne: Kaa Na Watu Wenye Uzoefu Wa Kuona Fursa.
Usiogope kuwaona watu wenye upeo mkubwa wa kuona fursa hasa wafanya biashara na wajasiriamali.
Mbinu unayoweza kuitumia kuongea naye ni hii: kama unaweza kumwandalia chakula cha mchana au cha jioni andaa, kwa sababu unapomwandalia chakula anajisikia vizuri halafu atakupa kila alichonacho kuhusu fursa.
Lakini pia unaweza kutumia nafasi hii kumwomba ujiunge naye kwenye biashara yake hata kama bila malipo ili ujifunze. Akikuruhusu hata asipokulipa wewe jitolee kufanya kazi bure utajifunza mengi, hiyo nayo ni fursa tayari itakusaidia huko mbele ya safari yako.

Mahali
Unapoweza Kupata Mawazo ya Fursa Kwenye Intaneti
Kuna tovuti na blogu nyingi zinazotoa mafunzo
mbalimbali ya namna ya kuziona fursa. Hapa TANEHA ni moja ya blogu zinazotoa na kuelekeza namna ya kupata fursa. Kinachotakiwa
ni kujiunga kwa email yako kwenye mitandao hiyo. Kujiunga na ujaze email yako halafu utakuwa
unatumiwa makala mbalimbali za fursa. Mitandao mingine ni pamoja na www.morningtanzania.com , www.about.com
, www.richdad.com , www.tonyrobbins.com n.k
Nakutakia kila la kheri kwenye safari yako ya
mafanikio.
0 comments:
Chapisha Maoni