Kwenye maeneo mengi ya maisha yetu tunahitaji usawa, kwa sababu binadamu wote ni sawa, hivyo kila mtu anastahili kupata huduma sawa, hii ni kweli kabisa. Lakini kuna maeneo kwenye maisha yako ambayo huhitaji kabisa usawa na mtu mwingine yeyote. Yaani kwenye maeneo hayo ukikubali usawa tu umejipoteza mwenyewe.
Kwa mfano ukienda kwenye msitu na miti yote ikawa inalingana kwa kimo, utakachoona ni msitu
pekee. Lakini kama utafika kwenye msitu wenye miti mingi inayolingana, lakini kukawa na mti mmoja mrefu kuliko mingine, utaanza kuona mti ule kabla ya miti mingine.
Hivi ndivyo inavyopaswa kuwa kwenye kazi yako au biashara yako. usikubali kabisa kuwa na usawa na wengine kwa kazi unayofanya, masomo, mahusiano au biashara unayofanya.
Tafuta kuwa tofauti, tafuta kuwa bora zaidi na tafuta kufanya kwa kipekee.
Kwa kuwa kila unachofanya kila mtu anaweza kufanya, njia pekee ya kusimama ni kuwa tofauti na wengine wote.
Tafuta kuwa tofauti, tafuta kuwa bora zaidi na tafuta kufanya kwa kipekee.
Kwa kuwa kila unachofanya kila mtu anaweza kufanya, njia pekee ya kusimama ni kuwa tofauti na wengine wote.
Na uzuri ni kwamba unaweza kuwa tofauti, uamuzi ni wako wewe mwenyewe, kuamua kuweka ubunifu na kuongeza ubora ili kuboresha kile unachofanya zaidi. Na kipimo chako kikiwa ni kutoa huduma bora
kabisa kwa wengine.
kabisa kwa wengine.
UKWELI NI KWAMBA
kitu pekee kinachoonekana ni kile ambacho kipo tofauti na wengine. Kwenye dunia ya sasa ambayo watu wengi wanafanya unachofanya, njia pekee ya kusimama na kuonekana ni kuwa tofauti na wengine.
kitu pekee kinachoonekana ni kile ambacho kipo tofauti na wengine. Kwenye dunia ya sasa ambayo watu wengi wanafanya unachofanya, njia pekee ya kusimama na kuonekana ni kuwa tofauti na wengine.
Kila siku ongeza ubora na kuwa tofauti na wengine huku nikiweka mkazo katika kufanya kitu bora zaidi.
CHUKUA HII.
"In order to be irreplaceable one must always be different". - Coco Chanel
"In order to be irreplaceable one must always be different". - Coco Chanel
(Ili uwe wa kipekee na akosekane wa kuziba pengo lako, kuwa wa tofauti).
Usikubali kuwa sawa na wengine kwenye kazi yako au biashara yako. Kukubali kuwa sawa na wengine ni njia ya uhakika ya kushindwa, iepuke kwa kuamua kuwa tofauti, kuwa mbunifu na kuweka ubora.
0 comments:
Chapisha Maoni