Mtu yeyote ambaye amewahi kupanda mlima mrefu, kama Kilimanjaro au mwingine wowote, atakuambia kitu kimoja muhimu, hakujikuta tu yupo kileleni. Badala yake alianza kupiga hatua moja baada ya nyingine, na kidogo kidogo akapanda mpaka kufikia kileleni.
Huu ndio ukweli wa maisha, huwezi kuibukia kileleni, yaani ukajikuta tayari upo kileleni, hakujawahi kutokea muujiza wa aina hiyo. Unapiga hatua moja baada ya nyingine na hatimaye unafika kileleni, kama hutaacha.
Lakini tunapokuja kwenye maisha ya kawaida, hasa maisha ya zama hizi, watu wamekuwa wakifikiri
wanaweza kuibukia kileleni. Kwamba umeanza kazi na baada ya muda mfupi umepanda cheo na kuwa
nafasi za juu. Au umeanza biashara na baada ya miezi kadhaa unamiliki biashara kubwa sana na yenye mafanikio makubwa.
wanaweza kuibukia kileleni. Kwamba umeanza kazi na baada ya muda mfupi umepanda cheo na kuwa
nafasi za juu. Au umeanza biashara na baada ya miezi kadhaa unamiliki biashara kubwa sana na yenye mafanikio makubwa.
Hiki ni kitu ambacho wengi wamekuwa wakijidanganya
na imepelekea kukata tamaa hasa pale wanapokutana na uhalisia wa maisha.
Kama ilivyo kwenye kupanda mlima, njia siyo rahisi.
- Kwanza ni kupanda mlima, KUPANDA, nafikiri unaelewa vizuri ilivyo vigumu kupanda.
- Pili njia inakuwa na mawe, maana yake kuna vikwazo vingi utakutana navyo na,
- Tatu kuna kuchoka na kukata tamaa.
Hivyo ndivyo ilivyo kwenye maisha pia, chochote unachotaka hakitakuwa rahisi, utakutana na magumu, utakutana na changamoto na utakutana na hali nyingi za kukatisha tamaa. Lakini utakapojua kwamba hakuna njia nyingine ya uhakika ya kufika kileleni, utaendelea na safari yako.
Ndiyo tutakutana kileleni, kwenye kilele cha mafanikio. Ila hatutaibukia pale, badala yake tutapanda kidogo kidogo. Kwa kuwa tayari kuweka juhudi kubwa na kutokukata tamaa.
UKWELI NI KWAMBA Safari yako ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio haitakuwa rahisi, lakini hupaswi kuiacha safari hii. Usitegemee kuibukia kwenye kilele cha mafanikio, Jiandae kupanda hatua kwa hatua mpaka kufika kileleni. Hakikisha kuwa hakuna kitakachokutoa kwenye safari hii.
CHUKUA HII;
“Every mountain top is within reach if you just keep climbing.” ― Barry Finlay
(Unaweza kufikia kilele cha mlima wowote kama utaendelea kupanda bila ya kukata tamaa).
“Every mountain top is within reach if you just keep climbing.” ― Barry Finlay
(Unaweza kufikia kilele cha mlima wowote kama utaendelea kupanda bila ya kukata tamaa).
Mafanikio hayatokei kama ajali, bali yanatokana na juhudi unazoweka kwa muda mrefu, kama ilivyo kwenye kupanda mlima, hatua kwa hatua.
NAKUTAKIA SAFARI NJEMA YA KUELEKEA KWENYE KILELE CHA MAFANIKIO!!
0 comments:
Chapisha Maoni