SABABU KUU ZA WANAWAKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA NA MATIBABU YAKE.
Utafiti unaonyesha asilimia thelathini ya wanawake wenye umri wa kufanya mapenzi yaani kuanzia miaka 18 mpaka 59 wana tatizo la kuishiwa hamu ya kufanya tendo la ndoa na hili ndio tatizo lao kuu inapokuja wenye afya ya tendo la ndoa kitaalamu kama sexual health, hii ni moja ya sababu inayowafanya wanaume wengi wakimblie nje kulala na Malaya au wanawake wengine kwani wawanawake zao kila siku hutafuta sababu ya kutofanya tendo la ndoa.
Lakini tatizo hili ni tofauti kidogo kwa upande wa wanaume kwani ni vigumu sana mwanaume kukataa kufanya tendo la ndoa na pia wanaume wanaweza kupata hamu kwa kutumia vidonge tu vya aina Fulani lakini wanawake inahitaji mchanganyiko wa njia mbalimbali ili kuweza kutatua tatizo lao yaani njia za ushauri wa kitaalamu na dawa pia wakati mwingine.
Zifautazo ni sababu za kuishiwa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake;
Matatizo ya kisaikolojia;
Linapokuja swala la tendo la ndoa amani ya moyo na uhuru wa kiakili unachangia sana mtu kupata hamu hata kufika kileleni lakini hali huu huweza kua na vikwazo kama historia ya kulazimishwa kingono au kubakwa hapo kipindi cha nyuma, mawazo mengi hasa ya kazi, matatizo ya kifedha,
kutojiamini na kuhisi labda maumbile yake mwanamke hayavutii, magonjwa ya akili na mgandamizo wa mawazo, mtizamo hasi kuhusu ngono kwamba anahisi ni unyanyasaji wa kijinsia na kadhalika.
kutojiamini na kuhisi labda maumbile yake mwanamke hayavutii, magonjwa ya akili na mgandamizo wa mawazo, mtizamo hasi kuhusu ngono kwamba anahisi ni unyanyasaji wa kijinsia na kadhalika.
Matatizo ya kimahusiano;
hisia za mwanamke kwa mwanaume wake humfanya kose hamu kabisa ya kufanya ngono,
mfano mawasiliano mabovu kati ya wapenzi, ugomvi kati ya wapenzi ambao haujapata suluhisho, kutoaminiana kati ya wapenzi na kuisha kabisa kwa hisia za mapenzi ambazo mwanzoni zilikuepo, ndoa ya muda mrefu sana pia huchosha kabisa linapokuja swala la tendo la ndoa.
Matatizo wakati wa ngono ;
Kama mwanamke anasikia maumivu makali kipindi cha kufanya ngono hujikuta akipoteza hamu kabisa na hakuna siku moja ataweza kusikia hamu kabisa.
Matumizi ya dawa Fulani ;
Baadhi ya dawa mfano dawa za kifafa, dawa za kupunguza mgandamizo wa mawazo na dawa za presha ya damu hupunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa kiasi kikubwa.
Magonjwa;
Magonjwa mengi huchangia kuishiwa hamu ya kufanya tendo la ndoa mfano magonjwa yote yanayosababisha maumivu mfano maumivu makali ya joint, maumivu makali ya kifua, maumivu ya tumbo pia magonjwa ya mishipa ya fahamu, kisukari, ugonjwa wa presha na kadhalika.
.
Uchovu:
.
Uchovu:
Kufanya kazi nyingi na kurudi nyumbani usiku ukiwa umechoka, kazi ya kuwahudumia watoto kama kufua, vyombo, kupika na kadhalika huleta uchovu mwingi ambao hupoteza kabisa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Upasuaji;
upasuaji wowote unaohusu matiti ya mwanamke au sehemu zake za siri unaweza kuathiri kabisa uwezo wake wa kushiriki tendo la ndoa.
Tabia na maisha kwa ujumla ;
Knywaji wa pombe uliopitiliza na uvutaji wa sigara huathiri uwezo na hamu ya kushiriki tendo la ndoa japokua unywaji wa wine kidogo kama glass moja huleta hamu ya kushiriki kingono.
Mazoea ya kushiriki aina zingine za ngono ;
Kuna aina zingine za ngono ambazo si za kawaida mwanamke akishazoea inakua ngumu sana kuacha hata akiolewa inakua vigumu kushiriki ngono za kawaida mfano mazoea ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, kufanya ngono na wanawake wenzake, kufanya ngono na mtu zaidi ya mmoja mfano threesome au foursome.
Ujauzito na kunyonyesha:
Kua kuna mabadiliko makubwa ya viwango vya homoni pale mwanamke anapobeba mimba na wakati wa kunyonyesha hii hupunguza hamu ya kufanya ngono kwa kiasi kikubwa sana.
Umri:
Kadri umri unavyozidi kwenda hamu ya kufanya ngono inazidi kupungua kwa wanawake na mwanamke anapofika miaka hamsini kitaalamu tunaita menopause homoni inayoitwa oestrogen hupungua sana na kumfanya awe na uke mkavu ambao hua na maumivu kipindi cha kushiriki ngono.
VIPIMO AMBAVYO HUFANYIKA
Kiwango cha homoni;
kupima kuangalia kama homoni za uzazi ziko kwnye kiwango sahihi
Pelvic examination;
Hii hupimwa na daktari kuangalia kama kuna tatizo kwenye viungo vya uzazi vinavyochangia tatizo labda uke kua mdogo sana na kuleta maumivu, ukavu wa uke na magonjwa ya viungo vya uzazi yanayoweza kuleta
maumivu kipindi cha tendo la ndoa.
maumivu kipindi cha tendo la ndoa.
MATIBABU
Ushauri;
Kama nilivyosema mwanzoni kuishiwa hamu ya kufanya ngono kwa wanawake huletwa na sababu nyingi na matibabu yake hutegemea sana chanzo cha tatizo husika yaani chanzo kikitatuliwa mtu ataweza kurudi katika hali yake ya kawaida. Mfano wanawake wenye matatizo ya kisaikolojia wanatakiwa wamuone mshauri aweze kuwasaidia kulingana na matatizo yao na kama kuna shida ya mahusiano kutafuta ufumbuzi
wake.
wake.
Matumizi ya dawa za homoni ;
Dawa za hormone zenye oestrogen peke yake au mchanganyiko wa oestrogen na progesterone husaidia sana kuongeza mzunguko wa damu kwa wanawake wenye matatizo ya homoni lakini pia wale ambao
umri umeenda kwani dawa hizi huongeza mzunguko wa damu kwenye sehemu za uke kupata hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Lakini pia cream za oestrogen na progesterone huweza kutumika pia kwa kupaka kwenye uke.
umri umeenda kwani dawa hizi huongeza mzunguko wa damu kwenye sehemu za uke kupata hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Lakini pia cream za oestrogen na progesterone huweza kutumika pia kwa kupaka kwenye uke.
Matumizi ya mvinyo:
Mvinyo au wine ikitumika kwa kiasi kidogo labda glass moja au mbili huongeza msukumo wa damu kwenye kinembe cha mwanamke na kumletea hamu ya kufanya tendo la ndoa. Mfano amarula, red wine, white
wine na kadhalika.
wine na kadhalika.
Pata likizo na mapumziko ;
Si rahisi kulala na mtu kitanda kimoja na mazingira yaleyale kwa zaidi ya miaka kumi bila kuchokana na hali hii huwatokea sana wana ndoa..hebu jaribuni kusafiri pamoja kubadilisha mazingira na kushiriki tendo la ndoa kwenye mazingira mapya wakati mwingine mwanamke aende kwa wazazi wake hata kwa wiki mbili mpaka tatu kwa mwaka kutembea ili mpate nafasi ya kukumkumbukana.
MWISHO ;
Mchanganyiko wa njia nilizotaja hapo juu zinaweza kusaidia sana kuliko kuchagua njia moja tu, hivyo unaweza ukatumia njia tofauti tofauti hapo ili kupata suluhisho la kudumu japokua virutubisho vya multimaca zimeonyesha uwezo wa hali ya juu ya kutibu tatizo hilo. kama uko kwenye mahusiano ambayo unajua kabisa
moyo wako haupo hapo au hisia zimekwisha hasa kabla ya ndoa ni bora kua muwazi tu na kuvunja
mahusiano kuliko kuendelea kudanganyana kwani huko mbele ya safari itakua taabu zaidi na usiolewe kumridhisha mtu, olewa kwasababu hisiazako ziko pale kwa uhakika.
moyo wako haupo hapo au hisia zimekwisha hasa kabla ya ndoa ni bora kua muwazi tu na kuvunja
mahusiano kuliko kuendelea kudanganyana kwani huko mbele ya safari itakua taabu zaidi na usiolewe kumridhisha mtu, olewa kwasababu hisiazako ziko pale kwa uhakika.
0 comments:
Chapisha Maoni