Jumatatu, 28 Machi 2016

Je Hisia Zako Zinatawala Akili Yako? Hiyo ni Hatari! Rekebisha

Kuongozwa na hisia badala ya akili ni lazima utakuwa ni mtu usiye na msimamo katika maisha yako. Leo utapanga hiki na kesho utapanga kile lakini hutatimiza hata moja au hata kama utatimiza ni kwa kuchelewa sana. 
Mambo mengi ya maana utayapuuzia kwa sababu akili haitakuwa na nguvu ya kutenda unachokitaka na badala yake hisia za wakati ule ndizo zitakazoamua nini ukifanye. Chukulia kwa mfano: Unaongozwa na hisia ya ulevi, kila utakapoona pombe lazima utakunywa tu kwa sababu akili haina nguvu yakupinga. Ukilewa, na hisia ya ulevi ikiisha unaanza kujuta kwa nini umekunywa pombe. 
Vivyo hivyo na mambo mengine utajikuta unapelekeshwa na hisia zako badala ya akili zao, hapo kufanikiwa kwako ni shida sana.

Nini Ukifanye Ili Kutibu Ugonjwa Huu?
Kuifanya akili yako iwe na nguvu kuliko hisia zako sio jambo rahisi. Ni kazi ngumu sana. Inahitaji muda na ubunifu mkubwa ili kutibu ugonjwa huu. Jiulize ni mara ngapi umejikatalia au umejinyima kufanya mambo fulani lakini bila kujua umejikuta unarudia kufanya mambo yale yale usiyoyapenda? Umetumia mbinu ngani kuishinda hali hiyo lakini mpaka sasa
bado hujafanikiwa? Unafikiri dawa yake ni nini?

  Mimi ninapendekeza Tiba  Aina Mbili Kutibu Ugojnwa Huu.

Tiba ya kwanza; Fanya kikao kila siku na watu waliofanikiwa ili waiimarishe akili yako na kuzifisha hisia zako. Hii ni mbinu ngeni kabisa kwa watu wengi lakini ni mbinu kabambe kabisa ya kutibu ugonjwa wa kuongozwa na hisia badala ya akili. 
Unachotakiwa kufanya ni kuchagua watu wawili au watatu haijalishi umbali waliko hapa duniani, wewe ikifika kwa mfano jioni kabla ya kulala waarike watu hao kwenye kikao cha dakika kumi. Unatakiwa kuwaalika kwa njia ya taswira unawaita kwa maneno unawahoji kwa maneno tena kwa sauti kumbuka katika ulimwengu wa roho hakuna umbali. Unapofanya hivyo taratibu utaanza kuishi kama wao walivyoishi/wanavyoishi. 
Unapowaita kwenye kikao wataje mmoja mmoja kwa jina lake na umuulize yeye amewezaje kufika hapo alipofika? Tafakari juu ya maisha yao na ili uweze kutafakari juu ya maisha yao unatakiwa ufahamu kwa undani juu ya maisha yao. Mbinu hii ni mzuri sana kuua hisia zenye kukuharibu na huifanya akili yako ikuongoze badala ya kuongozwa na hisia.

Hii itakusaidia kuongezeka kwa kiwango kikubwa kuitumia akili yako kukuongoza badala ya kuongozwa na hisia zinazopeleka upotevuni.

Tiba Ya Pili: Jenga akili yako kwa kuangalia  video au kusoma vitabu au kwa kusikiliza rekodi za watu waliofanikiwa kila siku. Hakikisha unajiepusha kangalia mambo yanayochochea hisia zako kuwa na nguvu kuzidi akili yako. 
Hisia ikiwa na nguvu hata kama ni kwa mambo mazuri bado utakwama baadhi ya mambo muhimu ya kutumia akili. Kwahiyo kama una video ya mtu aliyefanikiwa iangalie mara kwa mara ili akili ipate nguvu na kuzipiku hisia. 
Mbinu hii unatakiwa uifanye kila siku ili kupata matokeo mazuri haraka, kushindwa kufanya hivyo utasahau na matokeo yake hisia zitakuongoza.

Usipoutibu Ugonjwa Huo Mapema Nini Kitafuata?
Jambo kubwa litakalokupata ni kuchelewa au kushindwa kabisa kufikia mafanikio yako. Utajifunza mengi hutafanyia kazi hata moja kwa sababu hisia zitakuwa zinakupangia jambo lingine la kufanya badala ya lile ulilojifunza. Pia utajifunza mambo mengi lakini utadharau mafunzo na kuanza kutafuta mengine huku wenzako wakiyafanyia kazi mafunzo yale yale na kufanikiwa.

0 comments: