Jumapili, 27 Machi 2016

Sababu nne za Kushindwa Kufikia Malengo




  • Je, wewe ni aina ya mtu ambaye ana mpango mkubwa lakini kamwe haelekei kufika popote na mpango huo?  
  • Je, huwa unfanya maazimio mwanzoni na baadae huyapuuza kabisa?  
  • Labda wewe huhisi kama maisha ni njia moja na wewe huwezi kukaa kwenye njia hiyo ili kuyafikia?

Kama unaweza kuhusiana na yoyote kati ya maswali hayo, Basi makala hii ni kwaajili yako.  

Hakuna shaka katika akili yangu kwamba ubongo wa binadamu una baadhi ya utaratibu wa “MFUMO WA KUTAFUTA LENGO” Thumuni letu  la
kwanza na lengo kuu bila shaka, ni kuishi: Hivyo, Tunahitaji chakula cha kutosha, maji na angalau namna ya makazi na baadhi ya mahitaji
muhimu.
 
Katika siku hii na umri huu, ni vigumu kwa mtu yeyote kuwa na upungufu mkubwa wa chakula na maji, angalau katika jamii ya magharibi au kwa mtu yeyote ambaye ana uwezo wa kusoma makala hii. Kwa sababu hiyo, hatufikirii sana kuhusu kuishi tu badala yake tunaweka malengo mengine kwa kwaajili yetu kuhusu maisha bora ya siku za usoni.
Yaweza  kuwa ni malengo tija, malengo ya michezo au hata malengo ya kifedha. Vyovyote yawavyo ni muhimu kwetu kuwa nayo.
 
Katika makala hii nataka kuangalia sababu kuu nne za watu kushindwa kufikia malengo yao. Natumaini kwamba baadhi ya pointi hizi zinaweza kusaidia kuamsha ari yako ambapo unaweza kuwa umekwenda vibaya.; 

Kupunguza Imani;
 
Wakati mwingine, ninaposhindwa kuyafikia mambo ninayoyataka kwenye maisha, ni kwasababu tu kuwa siamini kama naweza kutikiza matamanio yangu. Inawezakuwa ni kwa sababu marafiki zangu wananiambia kuwa siwezi kufanya kitu au imani yangu mwenyewe inayoegemea kwenye uzoefu wa zamani. Kwa namna yoyote ile, nitajikuta nakubaliana na marafiki zangu pamoja na imani yangu kwa kukubali kushindwa.

 "Kama unafikiri kwamba unaweza, au kwamba huwezi, kwa kawaida uko sawa" - Henry Ford

Kama ukianza kwa kuwa na mashaka juu uwezo wako mwenyewe, itakufanya ufike mbali kwa kukata tamaa kwa mpango wako na kisha uendelee na mabo mengine. Njia nzuri ya kuyavuka mpaka huu ni kwa kutafuta watu waliofanikiwa baada ya kuipitia njia hiyo kama unavyoipitia wewe.

Kuchagua Lengo baya;

Kusema kuwa umechagua lengo baya hakupaswi kutumika kama kisingizio cha kuwa mvivu au kutafuta njia rahisi ya wewe kukata tamaa. Kuchagua lengo baya kuanzia kuzungumziwa pale tu utakapoamua kweli kuchagua lengo baya. Lengo baya huja katika njia tofauti tofauti kama vile;

  • Kujaribu kufanya jambo kwa sababu tu watu wamekuambia.
  •  Kufanya Jambo ili kuwafurahisha wengine,Kulenga jambo ambalo hujali kama unaweza kulitimiza au la,
  • Kuwaiga wengine kwa sababu tu unadhani kuwa wako kwenye njia sahihi.
Kuna mifano zaidi ya hii, lakini haya ni baadhi ya tu ya mabo ya kawaida. njia nzuri ya kupata  lengo sahihi kwa ajili yako ni kuchukua kalamu na karatasi na kuanza kuandika mambo yote ungependa kufikia. Kama utafanya hivi kwa adabu na kwa muda kiasi, kutakuwa na kitu ambacho kitasimama, kitu ambacho utahisi ni sahihi. Hili pengine ni lengo sahihi kwako.

Kukosa Msimamo/Subira;
 
Mara baada ya kuamua juu ya lengo lako, basi usikubali kitu chochote kukaa katika njia yako. Yawezekana wakati mwingine kukutana na vikwazo vya kimaisha kama ambavyo ni lazima itakutokea, lakini baada ya kuyashughulikia, hakikisha unarejea kwenye njia ya kulifikia lengo lako.
Lazima ufahamu kuwa wakati unaendelea kupambana ili kufikia mafanikio ya lengo lako, kuna maisha mengine yanaendelea, hivyo changamoto za hapa na pale hazifai kukuondoa kwenye lengo lako, zishughulikie, na uendelee mbele.
  
Kuna Hakuna "Hatua nyingine," kama Hakuna “Mpango wa Utekelezaji”
Baadhi ya watu hujipangia tu lengo na kuliacha hivyo. Ni jambo ambalo wanaliweka nyuma ya akili zao na huchukua hatua wakati wakikumbuka. Hakuna haja ya kuwa na lengo kama huna mpango wa utekelezaji kwa ajili yako mwenyewe au angalau muda maalum ambao ungependa kukamilisha.
Watu wenye wengi wenye mafanikio, Kila asubuhi huipitia karatasi ambayo ina malengo ya makuu katika maisha. Kisha huweka mpango kazi kwa kila lengo moja linalolazimu kulifanyia kazi na kukamilisha  wakati wa mchana. Una uhuru kidogo kama ukifanya kazi mwenyewe, lakini kanuni ya kuweka mpango pamoja bado inatumika.

Fahamu  kwa ukweli kwamba kama wewe haujaweka malengo au maazimio kwa mambo fulani ya maisha yako, hayawezi kufika mbali na kufanikiwa kama unavyotaka yawe.

Je, kuna kingine ambachoumepata katika njia ya kufikia malengo yako? Ningependa kusikia nyongeza yako katika comments!

0 comments: