Dalili, mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili zifuatazo,
kwa mwanaume hutokwa na manii zilizochanganyika na damu, kukojoa mkojo
mweusi au uliochanganyika na damu, kutoa mkojo kidogo sana tena kwa
shida, kukojoa mara kwa mara na kushindwa kumaliza mkojo wote.
Wengine
huona dalili za mkojo kujitokea wenyewe, hivyo mhusika kujikojolea,
kusikia maumivu wakati wa kukojoa au chini ya tumbo au kwenye kinena,
mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa na uume kuvimba.
Daktari akiona
moja ya dalili hizo mgonjwa anaweza kuchunguzwa kwa vipimo tofauti kama
vile kile cha kuchunguza mrija pamoja na kibofu cha mkojo (cystoscopy),
kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika kibofu baada ya mkojo
kutoka, X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram) atapimwa kama
ana magonjwa ya zinaa.
0 comments:
Chapisha Maoni