Polisi nchini Uganda inasema
imewakamata watu 103 katika maandamano yaliozuka kupinga kukamatwa kwa
mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi au Bobi Wine pamoja na wabunge
wengine kadhaana wanaharakati nchini Uganda.
Inaarifiwa pia mtu mmoja ameuawa katika purukushani hiyo.Vikosi vya usalama nchini Uganda vilizima maandamano kwenye mji mkuu hapo jana Kampala kupinga kukamatwa kwa Bobi Wine .
Waandamanaji wamechoma mot
o magurudumu ya magari, wanarusha mawe huku pia wakiweka vizuizi vya barabarani.
Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopita kufuatia madai kuwa alikuwa anamiliki silaha kinyume cha sheria.
Wengi wanayaona mashataka hayo kama yaliyochochewa kisiasa.
Misukosuko inaongezeka mjini Kampala kufuatia kukamatwa kwa mbunge Bobi Wine. Ripoti zimeibuka kuwa aliteswa akiwa mikononi mwa wanajeshi. Rais Yoweri Museveni amekana madai kuwa Bobi Wine alijeruhiwa.
Watu kadhaa wamekamatwa akiwemo mwandishi wa habari wa Reuters aliyekuwa akifuatilia ghasia hizo.
Wiki iliyopita Bobi Wine 32, na watu wengine walishtakiwa baada ya kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo eneo la Arua kaskazini mwa nchi. Polisi wanasema walikuwa wamewaongoza wafuasi wao kushambulia msafara wa Rais Museveni.
0 comments:
Chapisha Maoni