Kampuni ya Saruji ya Dangote Tanzania imedhamiria
kukabiliana na uhaba huo ikipanga kuzalisha zaidi ya tani 6,000 kwa
siku kutoka chini ya tani 3,000 za sasa.
Kampuni hiyo imesaini mkataba wa kuuziwa gesi asilia kwa miaka 20. Kampuni hiyo inayomilikiwa na bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote wa Nigeria na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Kabla ya ahadi hiyo itakayoanza kutekelezwa katika
miezi ya hivi karibuni, Dangote ilikuwa inatumia nishati ya dizeli kiasi cha lita 160,000 kwa siku ili kuzalisha tani 2,000 hadi 2,500 kwa siku, hivyo kugeuka mzigo mkubwa katika uzalishaji.
Hata hivyo, ili kupunguza tatizo la uhaba wa saruji lililojitokeza hivi karibuni, kampuni hiyo iliongeza uzalishaji na kufikia tani 3,300 badala ya zile za siku zote tani 2,000.
Utiaji saini mkataba wa mauziano ya gesi asilia yalifanyika Dar es Salaam jana baina ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Dangote Tanzania, Jagat Singh Rathee na Kaimu Mkurugenzi wa TPDC, Kapulya Musomba.
Kwa kuanzia, TPDC itaiuzia Dangote gesi ya ujazo wa futi milioni nane. Rathee amesema tatizo kubwa lililokuwa likikabili uzalishaji wa saruji kwa kiwanda hicho ni gharama kubwa za uzalishaji kwa kutumia umeme unaotokana na nishati ya dizeli.
Amesema uzalishaji saruji kutokana na nishati ya gesi utaanza ndani ya siku 45 na kwamba sasa wanamalizia ujenzi wa kuingiza gesi hiyo na kuzalisha megawati 35 za umeme kwa kuanzia na baadaye kufikia megawati 45 za umeme zitakazosaidia kuzalisha saruji kwa bei nafuu.
Alisema katika upatikanaji wa gesi asilia itasaidia katika uzalishaji wa uhakika, utunzaji wa mazingira, kuhakikisha msaada huo unakuwa na manufaa kwa Tanzania na kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Nigeria.
Musomba alisema matumizi ya gesi asilia katika kiwanda hicho ni katika awamu mbili ile ya kuzalisha umeme ambapo miundombinu iko tayari na awamu ya pili kuchoma udongo na tayari imekamilika.
Amesema katika kukamilisha Tanzania ya viwanda, wanatimiza wajibu wao kwa wakati na kufuata taratibu za nchi mpaka sasa Dangote kinakuwa kiwanda cha 42 kuzalisha kwa kutumia gesi asilia huku katika mwaka huu wa fedha wakitarajia kuongeza viwanda vingine saba.
Musomba amesema katika mkataba huo wa miaka 20 kwa kuwauzia gesi ya ujazo wa futi za ujazo milioni nane kwa awamu ya kwanza huku awamu ya pili ikizidi futi za ujazo milioni ishirini huku bei ya kuuziana itapangwa na mdhibiti, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Umeme (EWURA).
Amesema mpaka sasa kabla ya kuingizwa kwa Dangote viwanda vinavyotumia gesi asilia vilikuwa vikitumia gesi asilia za futi za ujazo milioni 15 mpaka milioni 17 na Dangote itaongeza matumizi ya viwandani na kufikia futi za ujazo milioni 23 na baada ya ya miaka miwili viwanda vyote vitakuwa vikitumia futi za ujazo milioni 40.
Amesema nchini gesi asilia imeanza kutumika mwaka 2004, lakini viwanda vimeanza kutumia gesi katika mwaka wa fedha 2006/07 kwa ushirikiano na kampuni ya Pan-African, lakini sasa uunganishaji gesi viwandani unafanywa na TPDC wenyewe.
Amesema kiwanda cha Dangote ni cha pili kikitanguliwa na kile cha Goodwill cha Mkuranga, ndivyo vilikuwa vikiendeshwa na TPDC wenyewe.
Hivi karibuni uhaba wa saruji uliingia Tanzania na kusababisha bei kupaa mpaka Sh 24,000 kwa mfuko, jambo lililomlazimu Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya kufanya mkutano na wazalishaji, wasambazaji, wasafirishaji wa saruji na kampuni zinazozalisha makaa ya mawe.
Manyanya aliwapa mwongozo wazalishaji hao kwa kuanza kuelezea kiwango cha saruji walichokuwa wakizalisha kwenye uzalishaji wa kawaida na kisha kuelezea kiwango ambacho ndani ya wiki hii wamekuwa wakizalisha.
Baadhi ya wawakilishi wa viwanda hicho walieleza changamoto wanazokabiliana nazo, akiwemo Meneja Mkuu wa Twiga Cement, Alfonso Velez ambaye alifafanua kuwa kiwango cha uzalishaji kilishuka kutokana na kuzima mitambo ya mwezi uliopita kwa ajili ya matengenezo lakini kwa sasa uzalishaji umerejea kama kawaida.
Mwakilishi wa Tanga Cement, Benedict Lema ambaye alikiri kushuka kwa kiwango cha uzalishaji kwenye kiwanda chake, alisema katika uzalishaji wa kawaida kiwanda kinaweza kuzalisha 3,500 hadi 4,000 kwa siku na hutumia tani 600 za makaa ya mawe kuendesha mtambo wa kuzalisha kiasi hicho cha saruji.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji kutoka Shirika la Madini ya Taifa (Stamico), Alex Rutagwelela alibainisha ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa makaa ya mawe, mwezi ujao itaanza kuzalisha tani 18,000 katika Kijiji cha Kaburo wilayani Ileje.
Mwaka jana, Waziri wa viwanda na Biashara, Charles Mwijage alisema viwanda vya saruji nchini vinatarajiwa kuongeza uzalishaji maradufu kutoka tani milioni 10.8 za wakati huo hadi kufikia tani milioni 20 kwa mwaka.
Alisema kuna viwanda vya saruji takribani 11 ambavyo vina uwezo wa kuzalisha tani milioni 10.8 wakati mahitaji halisi yaa nchini pekee ni tani milioni 4.7 kwa mwaka.
Anasema kuongezeka kwa uwezo wa uzalishaji wa tani za ziada umelenga katika kuhakikisha wanayateka masoko yaliyoko katika nchi za Afrika Mashariki, Afrika yote na hata nje ya Afrika, hasa nchi za Uarabuni.

0 comments:
Chapisha Maoni