Fahamu kuhusu ajira kwa watoto, ni
nini sheria inaseme kuhusu ajira kwa watoto na adhabu kwa mtu atakaeajiri
watoto katika kazi zake, fahamu pia sheria inamuelezea vipi mtoto, je mtoto ni
mtu wa aina gani?
- Je Sheria za kazi zinamuelezea vipi
mtoto?
Kifungu cha 4 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka, 2004
kinamuelezea mtoto kama mtu mwenye umri chini ya miaka 14 isipokuwa kwa ajira
zilizo katika sekta hatarishi, mtoto maana yake ni
mtu mwenye umri wa
chini ya miaka 18.
- Je kuna sheria yeyote inayosimamia
ajira kwa watoto?
Ndio, kuna sheria kadha wa kadha zinazoelezea ajira kwa watoto kama vile katiba
ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sheria ya Watoto na sheria ya
elimu na mafunzo ya ufundi stadi zikiwa ni miongoni mwa nyingi. Lakini
linapokuja suala la ajira na kazi, Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya
mwaka 2004 ndio inayokidhi hasa.
- Je kuajiri mtoto inakubalika
kisheria?
Kwa ufupi sheria inakataza mtoto mwenye umri chini ya miaka 14 kuajiriwa.
Sheria pia inaendelea kukataza ajira kwa watoto chini ya miaka 18 katika maeneo
ya migodi, viwanda, kama mabaharia katika meli au kazi nyingine yeyote
inayotambulika kua hatarishi. Hata hivyo, sheria inaruhusu ajira kwa watoto wa
miaka 14 katika kazi nyepesi ambazo sio hatarishi kwa afya ya watoto na
maendeleo na haihatarishi mahudhurio ya watoto shuleni, ,mafunzoni au programu
za kujifunza. Kwa ujumla ustawi wa watoto hautakiwi kuhatarishwa hata kidogo.
- Je kuna adhabu kwa mtu atakayeajiri
watoto kinyume cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004?
Ni kosa kuajiri watoto kinyume na sheria ya kazi inavyosema na adhabu inatolewa
chini ya kifungu cha 102 (2) ambacho kinampaHakimu wa Wilaya na Mkazi kutoa
adhabu sawa na faini isiyozidi shilingi milioni 5 au kifungo cha mwaka mmoja au
vyote faini na kifungo kama mahakama itavyoona inafaa, kutegemea na mazingira
ya kesi yenyewe.
-
Ni vipi Waajiri watafahamu kua maeneo yao ya kazi ni hatarishi?
Sheria inamtaka Waziri kuandaa orodha ya sekta hatarishi na kuisambaza kwa
umma. Kwa sasa kuna rasimu ya orodha hiyo kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira
lakini bado haijasambazwa na kua rasmi.
- Je mwajiri atakua na makosa kwa
kuajiri mtoto kwa kupewa taarifa zisizo sahihi au kutotambua?
Kama mwajiri atatoa madai kwamba hakufahamu kwamba mtu aliyemuajiri ni mtoto
wakati wa kumpa ajira au kudai kupewa taarifa zisizo sahihi watakua na wajibu
wa kuthibitisha kua ilikua sahihi kwa wao au mtu mwingine yeyote mwenye akili
timamu kuamini kwamba mtoto huyo alikua na umri wa kuajiriwa. Ni lazima
waonyeshe kwamba kulikua na hatua za kutosha kuhakikisha hawaajiri watoto.
Uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa, kumbukumbu za usahili na wazazi wa mtoto na
uthibitisho mwingine wowote kuonyesha kwamba walipotoshwa, hii itawasaidia
kuwaepusha na adhabu iliyotajwa hapo juu.
- Je mtu atakua na makosa kwa
kukuwadia mtoto kwa ajira?
Sheria inakataza kuajiri mtoto na kukuwadia mtoto kwa ajira. Kama kutakua na
uthibitisho kwamba kulikua na ukuwadi wa watoto kwa ajira basi mtu huyo atakua
na makosa na atachukuliwa hatua sawa na Yule aliyeajiri mtoto au watoto katika
maeneo yake ya kazi.
0 comments:
Chapisha Maoni