Rushwa ni kitu ambacho kinatolewa ili uweze kupata kitu Fulani au
kuhudumiwa kwa haraka kwa kutofuata utaratibu unaotakiwa kisheria au
kihalali.
Rushwa inaweza kuwa ni fedha, ngono, au uwajibikaji wa kazi Fulani.
Tunaporudi katika eneo la kazi Rushwa ipo katika njia 3:
1. Ngono
Suala la ngono limekua likiwatesa sana mabinti wengi kushinda wanaume
hasa katika upatikanaji mzima wa kazi au kazi kwa vitendo wanapokua
katika masomo yao, hasa ya elimu ya juu.Vile vile katika suala la
uongezaji wa mishahara wapo baadhi ya mabosi au waajiri wanaotaka kwanza
ngono ndipo waongeze mishahara au kumpandisha cheo mfanyakazi.
2. Fedha/Kitu cha Thamani
Kuna baadhi ya watu hupendelea kupewa fedha au kitu cha thamani ili
waweze kutoa haki ya msingi kwa mhitaji.Na fedha hutolewa ili watu
waweze kupata kazi,kupendelewa au kupunguziwa majukumu ya kazi,
kupandishwa cheo au kukwepa majukumu Fulani.Pia waajiri wengine au
waidhinishaji wa ajira (baadhi yao ) wamekua wakiendekeza suala la
kupokea vitu vya thamani kama njia ya kumuidhinisha mtu apate kazi.
3. Ngono na Fedha/ Kitu cha thamani
Kwa wakati mwingine rushwa ya ngono, fedha au kitu cha thamani inatumika kwa wakati mmoja(hutolewa) katika eneo la kazi.
NI KWA NAMNA GANI RUSHWA HII INACHUKUA NAFASI?
- Pale panapokua na maombi ya kazi na endapo mwombaji anajuana na mwajiri(kutokujiamini kwa baadhi ya waombaji wa kazi mara nyingi hupelekea hali hii),
- Unapokua sio muwajibikaji wa majukumu yako. Pindi utakaapoonekana sio mtekelezaji mzuri wa wajibu, unajiweka katika wakati mgumu hasa pale unapofika hatua yakusimamishwa au kuachishwa kazi. Mara nyingi hatua hii inapelekea uombaji na utoaji wa rushwa tajwa hapo juu,
- Unapokiuka kanuni,sheria na taratibu za kiofisi mfano kupigana au kutoa kauli mbaya kwa wafanyakazi wengine n.k
- Kwa baadhi ya wafanyakazi kutojua haki zao pindi wanapokua katika eneo la kazi hivyo kupelekea kuwa na hofu Fulani ambayo ni rahisi kushawishika kutoa ngono pindi anapokosea na kutishiwa na mwajiriau mkuu wake wa kazi,
- Kuwa muwazi kupita kiasi kwa kutoa matatizo yako kwa mwajiri/mkuu wa kitengo unachofanyia kazi.Hapa nieleze wazi,kuna baadhi ya watu sio wavumilivu na ni rahisi kuweka mezani maisha yake yote,ugomvi na hata matatizo yake ya kifamilia.Kitendo hiki humpa mwanya msimuliwaji kukusaidia hivyo kupelekea urahisi wa wewe kutoa rushwa yoyote endapo ataomba baada ya kukusaidia,
ATHARI ZA RUSHWA KATIKA KAZI
- Uvunjwaji wa sheria,kanuni na taratibu za kazi
- Matatizo na kutokuelewana kwa baadhi ya wafanyakazi hasa panapokua na rushwa ya ngono (uhusiano wa kimapenzi) kwa mwajiri na mfanyakazi mara nyingi uwajibikaji unapungua au haufanyiki kabisa hivyo kupelekea ukwamishwaji wa kazi za wengine ( team work)
- Huduma nzuri kwa wateja kupungua hivo kua na athari moja kwa moja kwa kampuni au shirika.(Bad reputation)
- Utatuzi wa jambo kuchukua muda mrefu hivyo kusababisha hasara
- Kuwa na na tatizo la wafanyakazi kuacha kazi (Labour turnover),hii ina athari kubwa sana na husababisha hasara zisizoepukika.
NINI KIFANYIKE?
- Kila mtu anatakiwa ajiamini hasa unapoomba kazi (mfano una elimu,na una nia na lengo why should you fear?) siku zote kuna kupata au kukosa. So have confidence.Tusijirahisishe kuwa watoaji wa rushwa mbalimbali,
- Waajiri wawe wanatoa kanuni, sheria na taratibu za kufanya kazi ikiwemo haki za mfanyakazi.(hii itamsaidia mtu kujua wajibu na mipaka yake ya kazi),
- Mfanyakazi kuwajibika ipasavyo na kwa wakati,
- Kutenganisha mambo yakifamilia na ya kazi,eneo la kazi iwe ni kazi na si mahala pakuzungumzia matatizo yako tu.(tuwe wasiri)
- Tuwe na mkakati binafsi wakutokutoa wala kuomba rushwa katika shughuli yoyote.
Wewe binafsi una njia au ushauri wowote katika kupambana na rushwa?
Tusifikirie katika kutoa adhabu kali tu bali katika kukataa na
kutokuomba.Shiriki katika hili kwa kuandika hapa totokomeze rushwa!!!!
0 comments:
Chapisha Maoni