Alhamisi, 23 Agosti 2018

JINSI YA KUFANYA MAHUSIANO YAKO KUWA BORA



Siku hizi kumekuwa na lawama nyingi kuhusiana na mahusiano ambapo kila upande umekuwa ukilaumu upande mwingine kuwa ndio chanzo cha kuvurugika kwa mahusiano yao, kibaya zaidi ni kwamba wakati mwingine upande unaokua unalalamika sana unaweza ukawa ndio upande uliochangia kwa kiasi kikubwa kuvurugika kwa uhusiano uliokuwepo
Japo kuna njia nyingi za kuboresha mahusiano kulingana na aina ya wahusika waliopo katika mahusiano, Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo unaweza kuzitumia kuboresha mahusiano yako.

1. Jitambue Wewe binafsi pamoja na kumtambua mwenzako
Siku zote katika maisha unatakiwa ujitambue
wewe ni mtu wa aina gani, unapenda vitu gani,  mipaka yako katika uvumilivu, vitu vinavyokukukasirisha kwa urahisi, udhaifu wako, uwezo wako kifikra pamoja na mambo mengine, kwa upande mwingine unatakiwa pia kufahamu aina ya mtu uliyenaye katika mahusiano, vitu gani anaweza kuvifanya anapokuwa amekasirika, vitu gani vinvyomkasirisha kwa urahisi, vitu gani vinavyomfurahisha, udhaifu wake, ubora wake na uwezo wake kifikra, kimawazo,  kishauri, mipaka ya uvumilivu wake pamoja na mitazamo na misimamo yake kuhusiana na maisha.

2. Kujenga utaratibu wa kutatua changamoto zenu wenyewe badala ya kuwategemea zaidi marafiki
Kila mahusiano yanajengwa kwa misingi na taratibu tofauti kulingana na aina ya watu waliopo katika hayo mahusiano, hivyo basi ni vizuri mkajenga utaratibu wenu wa Kushauriana mambo mbalimbali pamoja na kutatua changamoto zenu mbalimbali kupitia mazungumzo bila ya kuwepo kwa shinikizo lolote kutoka kwa marafiki zenu, hii itawasaidia Sana kudumisha mahusiano yenu pamoja na kutengeneza urafiki baina yenu, mnapowategemea sana marafiki zenu kuendesha uhusiano wenu mnaweza mkachangia marafiki zenu watengeneze mahusiano na watu mlionao katika mahusiano baada ya kuwa karibu nao sana.

3.Tumieni mda mwingi kuongelea mambo yanayowahusu badala ya kuwaongelea watu wengine
Kila Mwanadamu amezungukwa na changamoto mbalimbali za kimaisha pamoja na malengo mbalimbali anayoyatamani kuyafikia, mnapokuwa mmejenga utaratibu wa kazungumzia mambo yenu pamoja na kushirikiana kwa pamoja katika kutimiza malengo ya kila mmoja na hivyo kupelekea mzidi kuwa karibu, inapotokea unapenda kuongelea mambo ya watu zaidi inakuwa ni vigumu kuambiwa mipango ya mtu uliyenaye katika mahusiano kwa kuogopa hiyo mipango kuvuja kwa watu wengine kabla haijafanikiwa.

4 . Kujijengea utaratibu wa kutunza siri zenu
Inapotokea mtu anakuwa wazi katika mahusiano yenu basi unatakiwa uhakikishe kuwa mambo anayokueleza hayatoki nje ya nyingi mlio katika mahusiano na inapotokea mwenzako ana matatizo basi akikisheni mnatatua hayo matatizo katika namna ambayo haiwezi kumvunjia heshima, Siku zote unapoaminiwa jitahidi kuaminika.

5. Jijengee Utaratibu wa Kushauri  mambo ya kimaendeleo badala ya starehe
Kila mmoja anapenda kuishi katika maisha mazuri pamoja na kutimiza malengo na ndoto alizojiwekea, ili hivi vitu vyote viweze kutimia ni lazima huyo mtu azungukwe na mtu/watu ambao watakuwa wanamshauri pamoja na kumpa moyo katika safari yake ya kutimiza ndoto zake au aamue mwenyewe kuangaika na kujituma katika kufanikisha ndoto zake, ili uwe katika nafasi nzuri ya kuboresha mahusiano yako ni vizuri ukajikita zaidi katika kumshauri mwenza wako zaidi katika masuala ya kimaendeleo badala ya starehe ambazo hazina faida yoyote.

6.Jiheshimu pamoja na kujenga mazingira ya kuheshimika wewe na uliyenaye katika mahusiano
Usipende kazungumzia madhaifu ya mtu ambaye upo nae katika mahusiano kwani hayo yanaweza yanachangia kwa kiasi kikubwa wewe pamoja na mtu uliyenaye katika mahusiano kudharaulika na watu mbalimbali, wewe binafsi utonekana mjinga kwa kushindwa kutunza siri za mwenza wako pia epuka kufanya mambo ambayo yanaweza kukudhalilisha mbele ya watu pamoja na kumdhalilisha mwenzako.

0 comments: