Jumamosi, 12 Machi 2016

HATUA MUHIMU

Mambo 10 Rahisi Unayoweza Kuanza Kufanya Leo Na Ukaboresha Maisha Yako.

Safari ya maisha ni safari yenye changamoto nyingi sana. Katika safari hii kuna milima na mabonde na hata visiki vinavyoweza kukukwamisha. Ili kuweza kushinda changamoto hizi kuna vitu vidogo vidogo sana unavyoweza kufanya kila siku na ukaboresha maisha yako.

Haya hapa ni mambo 10 unayoweza kuanza leo na ukaboresha maisha yako.

1. Kuwa na mtazamo chanya. Katika kila jambo linalotokea jua kuna kitu kizuri cha kujifunza au
kunufaika. 

2. Kunywa maji mengi. Sehemu kubwa ya mwili wako ni maji, ukosefu wa maji unaweza
kukufanya upate matatizo ya kiafya.
3. Jenga tabia ya kujisomea. Tabia hii itakufanya uweze kufikiri
zaidi na pia utajifunza zaidi. Kuna vitabu na machapisho mbalimbali yanayoweza kukujenga kifikra.

4. Jifunze kusema hapana.
Matatizo mengi unayokutana nayo kwenye maisha yako yanatokana na wewe kukubali kila kitu unachokutana nacho au unachoambiwa. Anza leo
kusema hapana.

5. Acha kutumia simu yako kwa
muda. Simu za kisasa zimetufanya tuwe watumwa wa kila mara kuangalia nini kinaendelea. Anza leo
kuzima simu yako japo kwa saa moja na utumie muda huu kufanya mambo mengine.

6. Pata kifungua kinywa.
Watu wengi wanakosa kifungua
kinywa kwa sababu ya haraka au kupunguza matumizi, usifanye hivi.

7. Usitumie zaidi ya unachopata, hakikisha matumizi yako yanakuwa
pungufu ya kipato chako.

8. Acha kulalamika.
Kama kuna kitu hukipendi kibadilishe, kama huwezi kukibadilisha achana nacho.

9. Omba msaada. Huwezi kufanya kila kitu wewe mwenyewe, unahitaji
msaada wa watu wengi.

10. Kaa mbali na watu wenye kukatisha tamaa. Ukiwa karibu nao
watakurudisha nyuma. Maisha unayoishi ni yako na una uwezo wa kuyabadili na kuyafanya vile
unavyotaka wewe.

Anza leo kwa kufanya mambo
hayo rahisi na utaona mabadiliko makubwa.

* endelea kupitia blog hii kwa muendelezona uchambuzi wamambo yote kumi na ufafanuzi wake.

0 comments: