Hakuna wakati mzuri wa kupima ukuaji wetu, kupima maendeleo yetu binafsi kama wakati ambapo tunapitia changamoto.
Mambo yanapokuwa shwari hakuna tatizo, kila kitu kinakwenda kilivyopangwa na hata mtu wa kawaida ataonekana ni bora kwenye nyakati hizo.
Lakini mambo yanapokuwa magumu, changamoto zinapoibuka, hapa ndipo tunapowajua wale wa tofauti, wale waliojitoa kweli na wale ambao wapo wapo tu.
Na katika changamoto yoyote kuna njia mbili za kupambana nayo, kuna njia rahisi na kuna njia sahihi. Hizi ni njia mbili tofauti kabisa, na haziwezi kuwa pamoja, ni unachagua kufanya kilicho rahisi au kufanya kilicho sahihi.
Wakati wa changamoto kuna njia nyingi rahisi kuchukua. Kukataa changamoto, kutafuta mtu wa kumlaumu juu ya changamoto hiyo, kukata tamaa na k
uacha na kuamua kuiacha mpaka itakapoondoka yenyewe. Njia rahisi inaweza kuwa rahisi sasa, lakini baadaye ina madhara makubwa sana.
Pia wakati wa changamoto kuna njia sahihi za kuchukua, kutafuta kiini cha changamoto, kujiuliza umechangiaje changamoto hiyo na kujitoa kuifanyia kazi changamoto ili uweze kusonga mbele. Njia sahihi ni ngumu mwanzoni ila ina manufaa makubwa sana kwa baadaye.
Mara zote unapojikuta kwenye changamoto, au unapokuwa njia panda, na kuna njia rahisi na njia sahihi, chukua njia sahihi. Usijali inakuumizaje kwa sasa, njia sahihi ndiyo itakayokutoa, nyingine zitakupotezea tu muda na nguvu zako.
UKWELI NI KWAMBA kwenye changamoto Unazokutana nazo, kuna njia rahisi na njia sahihi. Njia rahisi ni rahisi mwanzoni lakini baadaye inakuletea changamoto zaidi. Na njia sahihi ni ngumu mwanzoni lakini itakuletea faida kubwa zaidi. Kuanzia sasa chukua njia sahihi, bila ya kujali upo kwenye mazingira gani.
CHUKUA HII
Have the courage to say no. Have the courage to face the truth. Do the right thing because it is right. These are the magic keys to living your life with integrity. - W. Clement Stone
Have the courage to say no. Have the courage to face the truth. Do the right thing because it is right. These are the magic keys to living your life with integrity. - W. Clement Stone
(Kuwa na ujasiri wa kusema hapana. Kuwa na ujasiri wa kukubali ukweli. Fanya kilicho sahihi kwa sababu ni sahihi. Hizi ni funguo za kuishi maisha ya uadilifu).
Mara zote fanya kile ambacho ni sahihi, usikimbilie kufanya kile ambacho ni rahisi.
Rafiki na Kocha Wako,
Rafiki na Kocha Wako,
0 comments:
Chapisha Maoni