Katika kila jambo linaloendelea duniani, kuna makundi mawili ya watu. Kuna walaji na kuna wazalishaji.
Walaji ni wale ambao wanasubiri kitu kitoke na wao waanze kutumia.
Walaji ni wale ambao wanasubiri kitu kitoke na wao waanze kutumia.
Na wazalishaji ni wale ambao wanaangalia kipi kinahitajika na wanakitengeneza kisha kuwapatia walaji.
Katika makundi haya mawili wanaonufaika zaidi ni wazalishaji, kwa sababu walaji wanahitaji kuingia gharama kupata kile kilichozalishwa. Kila mmoja wetu ni mlaji kwa vitu fulani, kwa sababu hatuwezi kuzalisha kila kitu sisi wenyewe.
Lakini cha kusikitisha kuna wengi ambao siyo wazalishaji, au wanazalisha
kidogo sana. Na wanaishia kuwa walaji wakubwa, kitu ambacho kinawafanya waishi maisha magumu sana.
Hakikisha unakuwa mzalishaji mzuri kwenye maeneo ambayo umechagua wewe mwenyewe.
Usifurahie tu kuwa mlaji, bali jiulize na wewe umezalisha nini.
Usifurahie tu kuwa mlaji, bali jiulize na wewe umezalisha nini.
Kwa mfano tukija kwenye hii teknolojia ya mitandao ya kijamii, ambayo inakua kwa kasi sana, wengi wanaishia kuwa walaji. Kwamba wanafurahia kutumia kila mtandao wa kijamii, lakini hawajiulizi ni kwa namba gani wanaweza kutumia mitandao hiyo kuzalisha pia.
Wewe usiishie tu kuwa mtumiaji wa mitandao hii, fikiria pia ni kwa jinsi gani unaweza kuitumia kuzalisha zaidi ili uweze kuongeza thamani kwa wengine na wao wakupe wewe fedha.
UKWELI NI KWAMBA kuna makundi mawili ya watu, walaji na wazalishaji. Walaji wanafurahia kutumia vitu na wazalishaji wanatengeneza vitu kwa ajili ya wengine. Pamoja na kwamba utakuwa mlaji, lakini pia hakikisha ukuwa mzalishaji mzuri na kuhakikisha unatoa kitu chenye thamani kubwa kwa wengine.
CHUKUA HII
“Happy people produce. Bored people consume.” ― Stephen Richards
(Watu wenye furaha wanazalisha. Watu waliochoka wanatumia).
“Happy people produce. Bored people consume.” ― Stephen Richards
(Watu wenye furaha wanazalisha. Watu waliochoka wanatumia).
Hakikisha huishii tu kuwa mlaji, badala yake unazalisha pia. Unapozalisha unaongeza thamani kwa wengine na kwako pia, na hii itakuletea furaha.
0 comments:
Chapisha Maoni