Kuweka malengo, uaminifu, nidhamu, kufanya kazi kwa bidii na kuipenda kazi yako ndio siri pekee ya mafanikio ulimwenguni. Kuweka malengo ya kukuza uchumi ndio dira pekee itakayokupeleka katika kilele cha mafanikio, weka malengo yako kwa kuyagawanya katika sehemu tatu, Malengo ya muda mfupi, ya kati na ya muda mrefu.
Ni muhimu kupitia malengo yako anagalau mara moja kila mwaka. Hii itakusaidia kufanya mabadiriko katika orodha ya malengo yako, pia itakusaidia kuondoa orodha ya malengo yaliyokwisha timizwa.
Watu hutumia njia mbalimbali kupanga malengo yao ,
lakini leo hii nitakuonyesha njia rahisi ya kupanga na kuboresha
male
ngo yako kiuchumi.1. Malengo ya muda mfupi (Mwaka 1 hadi 2)
Mfano;-
- Kutenga pesa ya dharula.
- Maandalizi ya harusi.
- Kujiunga na elimu ya juu.
- Kumsaidia mwana familia.
- Kununua thamani za ndani kama vile, kompyuta, radiao n.k
2. Malengo ya kati (Miaka 2 hadi 5)
Mfano;-
- Kuanzisha familia.
- Kununua uwanja na kujenga nyumba au kununua nyumba.
- Kununua chombo cha usafiri kama vile gari.
- Kupanga ziara ya mwaka.
- Kupunguza madeni.
- Kutenga kiwango Fulani cha pesa kwaajiri ya maandalio ya kustaafu.
3. Malengo ya muda mrefu (Miaka 5 hadi 10).
Mfano;-
- Kuanzisha bihashara kubwa.
- Kujenga nyumba ya kifahari.
- Kuanza kutenga pesa kwaajiri ya elimu ya watoto.
Baada ya
kuboresha malengo yako ya kifedha, mikakati mathubuti inatakiwa
kupangwa kuhakikisha kuwa unafanikisha malengo yako. Kuweka malengo ya
kifedha kunakusaidia kuona picha kubwa ya maisha yako ya baadaye. Hivyo ni muhimu kuwa na mikakati ya kifedha katika maisha yako hata kabla haujaanza kuzalisha kiwango chochote cha pesa.
Ufuatao ni mfano wa jedwari la mikakati ya kifedha, litakalo kusaidia kukupa muongozo wa kuendesha mipango yako;-
MPANGO WA MUDA MFUPI | KIASI | HATUA |
Mf. Kutenga pesa ya dharula | Tshs.5,000,000/= | Imetimia |
MPANGO WA KATI | KIASI | HATUA |
Mf. Kununua kiwanja kwaajiri ya nyumba ya makazi | Tshs.10,000,000/= | Unaendelea – imetimia 50% |
MPANGO WA MUDA MREFU | KIASI | HATUA |
Kutenga pesa kwaajiri ya elimu ya watoto. | Tshs.10,000,000/= | Haujajanzishwa |
Baada kujifunza jinsi ya Kupanga malengo katika hatua ya kuboresha uchumi wako, ni muhimu sasa kutambua mambo muhimu utakayotakiwa kuyazingatia, ukitaka kutekeleza malengo yako, kama ifuatavyo;-
1. Fungua akaunti ambayo itakuwezesha kutunza na kukuza pesa ya kila lengo.
2. Weka mpango wa kutenga pesa, utakao kuwezesha kutimiza malengo yako.
3. Ni kiasi gani cha pesa kitatosheleza kutimiza kila lengo?
4. Ni kiasi gani cha muda kitatosheleza kufanikisha malengo yako?
5. Ni kiasi gani cha pesa kitahitajika kutengwa kila mwezi ili kufanikisha malengo yako?
0 comments:
Chapisha Maoni