Kama unapenda kufanikiwa
kimaisha nakuomba kwa unyenyekevu, asiwe miongoni mwa watu ambao
watakuwa na tabia zifuatzo kwani haweza kufanikiwa kimaisha.
- Hufikiri, kusema na kufanya yasiwezekane
Watu wasioweza kufanikiwa hujaa fikra za kutofanikiwa na mara nyingi
hulalamikia sana matatizo yao. Wakati mwingine wasioweza kufanikiwa
hugeuza mambo mema na kuyafanya yaonekane mabaya, jua likiwaka
watalalamika joto, likipoa watalaumu baridi,
watalaumu foleni za barabarani, yaani kwao kila jambo wataligeuza na
kulipa sababu mbaya. Hata wanaposhindwa
kutekeleza jambo hutoa sababu,
yote ni kuzilinda fikara zao za kutofanikiwa.
Tabia hii hukua mpaka kufikia hatua wanapowatazama wenzao hudhani
kuwa wanawasengenya, kuwafanyia mambo mabaya, kuwasaliti, ilimradi tu ni
kuwa kinyume na mambo mema. Watu wa namna hii hata kama watasaidiwa
namna gani hugeuza misaada hiyo kuwa ya kujipendekeza na mara nyingi
hupuuza wema haraka na kueneza mabaya ya mtu. Lakini pamoja na yote
kutokana na fikra zao kuwa za kushindwa watu wa tabia hii hukata tamaa
mapema, pale wanapofanya jambo na kuonekana lina ugumu kidogo.
- Hutenda kabla ya kufikiri
Tabia ya pili ya watu wasioweza kufanikiwa kimaisha ni hii ya kutenda
jambo kabla ya kufikiria. Watu wa aina hii, kuwa wepesi sana kununua
vitu barabarani mara tu wanaposhawashiwa na macho au wauzaji. Utakuta
mtu bila hata kujiuliza faida za kitu hicho anaamua haraka kukipata.
Ataamua kwa haraka kuoa, kuolewa, kukubali kujiingiza katika mapenzi na
hata kufanya jambo lo lote bila kujiuliza atanufaika vipi?
- Hupenda kuzungumza zaidi ya kusikiliza
Watu ambao wako katika hatari ya kutofanikiwa ni wale ambao daima ni
wazuri katika kuzungumza kuliko kusikiliza. Wao huwa ni wajuajia wa kila
kitu, hawako tayari kupokea ushauri. Siku zote wanapokuwa kwenye
makundi ya watu pengine wajuzi zaidi yao
wao huwa hodari kujenga hoja kutetea mambo yao hata kama hayafai.
Unaweza kumkuta mtu ni kiongozi wa ngazi za juu, amefanya kosa na watu
wote wameona kuwa kakosea lakini mhusika hujiona si mikosaji.
Mtu anapokuwa muongeaji sana huwa mgumu kupokea ushauri wa ye yote,
anachoamua yeye hukifanya kwa imani kuwa kinafaa. Ukiwa mtu mwenya tabia
ya aina hii huwezi kufanikiwa kabisa katika maisha yako. Watafiti wa
masuala ya biashara ulimwengini waliwahi kushauri kuwa mipango mizuri ya
kibiashara hutoka kwa watu masikini, ambao walisema hufikiri zaidi
namna ya kujikomboa kuliko matajiri wanavyofikiri katika kujiendeleza,
hivyo wakasema kama mtu anataka kufanikiwa kibiashara lazima asikilize
mawazo ya masikini si kuwapuuza kwa kujiona ni bora zaidi yao.
- Hukata tamaa mapema
Watu wanaotaka kufanikiwa huchukulia ushindwa kama hatua ya kuelekea
kwenye mafanikio, lakini watu wasioweza kufanikiwa wanapojaribu mara
moja au mbili kuvuka kikwazo fulani cha kimaisha na kushindwa hukata
tamaa na kutotaka kujaribu tena kusonga mbele. Wanye tabia ya kushindwa
kimaisha hawako tayari kudumu na jambo moja linaloonekana kushindikana
kwao kwa muda mrefu. Akiona mwanamke ambaye ni mkorofi kidogo, haraka
hukimbilia kumwacha na kutafuta mwingine, mara nyingi si watu
wavumilivu.
Akijaribu biashara ya vitumbua kwa wiki moja na akaona havinunuliwi,
anaaza kupika maadazi, wiki moja baadaye yuko kwenye mihogo, basi
ilimradi ni kuhangaika kusikokuwa na tija katika maisha. Ukitaka kuwa
mmoja kati ya watu wasiweza kufanikiwa kimaisha, basi jaribu kuishi
maisha ya kukata tamaa mapema unapofanya mambo.
- Hujaribu kuwarudisha nyuma wengine
Wasioweza kufanikiwa katika maisha huwa na tabia moja ya ajabu ambayo
ilianzishwa na Hawa mwanamke anayetajwa katika Kitabu cha Biblia kuwa
ni mtu wa kwanza kufanya dhambi. Mwanamke huyu alipodanganywa na nyoka
na kuchuma tunda hakutosheka na dhambi zake, bali alimpelekea na mumewe
Adamu naye akala. Mara nyingi watu walioshindwa kimaisha kuwa na tabia
za kuwashawishi watu wengine wawe kama wao katika mawazo na matendo.
Tabia za watu wa aina hii huwa si za kimaendelezo kwa vile wao
hudhani kuwa njia zao ni sahihi na hivyo hujaribu kwa nguvu zao
kuwarudisha wengine nyuma ili wawe kama wao. Ni watu wenye wivu wa
‘kijinga’ wakiona mwingine anaendelea katika hiki na kile humpiga vita
ili afilisike. Ni wingi wa fitina, uchonganishi. Wenye tabia za
kutofanikiwa hudhani kuwa kukwama kwao hutokana na vikwazo vinavyoletwa
na wengine. “Kwa sababu jamaa kanikwamisha hiki na kile, nimkwama kwa
sababu ya kaka yangu”
- Hupoteza muda mwingi
Watu ambao hawawezi kufanikiwa ni wale ambao hupoteza muda mwingi
kufanya mambo yasiyokuwa na tija, kwa kuangalia Tv, kusengenya watu,
kunywa pombe, kufanya starehe na kutumia muda hovyo kwenye kazi ambazo
hazina msaada kwao. Wapo watu mahodari kutembelea kwenye nyumba za
wengine na kuongea huko kutwa nzima bila kujali kama muda waliopoteza
wangeweza kufanya kazi na kujipatia kipato.
- Huchagua mambo rahisi
Wakati mwingine mafanikio huhitaji kufanya kazi ngumu zenye kuchosha,
lakini watu wasiokuwa na uwezo wa kufanikiwa wanapoletewa mambo mawilii
huwa wepesi zaidi kuchagua jepesi kulifanya. Kama ni kazi, basi zisiwe
ngumu sana ziwe nyepesi nyepesi ambazo watazifanya bila jasho. Watu
wasiokuwa kwenye njia ya mafanikio hawapendi kujituma, wepesi kuchoka na
mara nyingi hupenda sana kufanya kazi kidogo na kulala sana.
Tabia za watu wasioweza kufanikiwa huwa ni za kukwepa kuwajibika.
Hata kama kuna mtu anataka kumpatia kitu na akamwambia awahi kesho yake
asubuhi, huchelewa kwa vile hawezi kujihimu asubuhi na kuacha raha ya
usingizi, wakati mwingine hata akiambiwa asubiri mpaka muda fulani huwa
hayuko tayari kusubiri.
0 comments:
Chapisha Maoni