Mungu anaupendeleo? Kwanini
kuna watu wanaitwa ma-genius na wengine wanakuwa sio ma-genius? Unafikiri
tofauti ni nini?. Je, wewe ni genius kama jibu ni ndiyo nakupongeza kama jibu ni
sio kwanini sio genius?
Wakati natafakari somo
hili nilishangaa sana kupata ufahamu ambao kipindi cha nyuma sikuwa nao.
Nilirejea historia ya watu mashuhuri duniani ambao wameweza kufanya mambo
makubwa yaliyosaidia kuufikisha ulimwengu mahali hapa. Baadhi yao ni akina Sir Isack Newton, akina Bill Gate, akina
Einstern Albert na wengine wengi. Ambao kila mmoja wao amefanya kitu cha
kipekee kilichoushangaza ulimwengu.
Kwa kifupi na kwa lugha
rahisi, neno Genius ni mtu ambaye
anauwezo wa kutumia akili yake kwa kiwango ambacho akili hiyo hiyo inampa
matokeo makubwa au anatengeneza matokeo makubwa. Kila mtu anaakili lakini namna
ya kuzitumia akili hizo tunatofautiana. Kwenye makala hii nalenga kuangalia
namna au njia sahihi ambayo mtu anaweza kufanya ili aweze kufikia kuwa genius au
aweze kujitengeneza yeye mwenyewe kuwa genius.
Chukulia kwa mfano; mimi
nimeajiriwa ninauhakika wa kupata mshahara wangu mwisho wa mwezi. Wewe
hujaajiriwa lakini unamiliki kampuni ya kutengeneza sabuni. Mimi nafanya kazi
kwa kufuata mwongozo nilioukuta ofisini nilipoajiriwa.
Wewe unajiandalia
mwongozo wako mwenyewe lakini pia ili upate wateja wengi wa sabuni ni lazima
ufanye ubunifu wa kipekee ili bidhaa yako iuzike sokoni haraka. Kwahiyo, wewe muda mwingi zaidi unatumia kufikiri jinsi
gani utapanua biashara yako lakini pia jinsi gani utaboresha bidhaa zako ili
ziuzike sokoni.
Bila shaka kwa sababu wewe ndiyo kila kitu kwenye kampuni yako,
utaishughulisha sana akili yako ili ikupe
matokeo makubwa, kadri unavyoendelea kupanua biashara yako na kadri
unavyoendelea kuboresha bidhaa zako ndivyo kiwango cha Ugenius kinavyoongezeka
kwako.
Hii ni tofauti kabisa na mimi niliyeajiriwa kwa sababu mimi nafanya kazi
kwa kutumia mwongozo ambao nimeukuta ofisini, akili yangu sitaitumia kwa
kiwango kikubwa kwani nafahamu hata kama mambo yasipoenda vizuri mshahara wangu
upo pale pale. Matokeo yake sasa; ni
vigumu sana mimi kuwa genius, zaidi
nitabaiki kuwa mtu wa kawaida tu.
Wasomi
Wetu Wako Wapi?
Kutokana na mfano huo hapo
juu utashangaa sana wale waliokuwa vichwa darasani au waliokuwa wanafanya
vizuri kwenye masomo, ugenius wao
hupotea haraka mara wapatapo kazi ya kuajiriwa. Hapa Tanzania tuna wasomi wengi
ambao walikuwa magenius darasani lakini sasa hivi wapo wapo tu utawakuta
wameshaajiriwa sehemu mbalimbali hawaishi kwa akili zao tena wanaishi kwa kufuata
miongozo na masharti ya waajiri wao ugenius wao haupo tena.
Mambo
Mawili Ya Kufanya Ili Kujitengeneza Kuwa Genius
Mambo yote yanawezekana
ukiamua, kama hujaamua kuwa genius makala hii haitakufaa kitu lakini kama
unakiu ya kuitumia akili yako ipasavyo ili ikuletee au ikutengenezee matokeo
makubwa, unao uwezo wa kufanya hivyo. Kuna mambo mawili unatakiwa kuyafanya ili
uweze kuwa genius mambo hayo ni haya yafuatayo;
Kiwango cha uhuru. Kujitengeneza
kuwa genius kwenye jambo lolote ni lazima uwe na uhuru wa kufanya hivyo.
Ninaposema uhuru maana yake upate muda wa kujiamulia mambo yako mwenyewe bila kutegemea
mtu mwingine. Unatakiwa kutafuta uhuru huo popote hapo ulipo. Unapokuwa na
uhuru wa kufikiria na kufanya chochote upendacho hiyo ni hatua nzuri inayoweza
kukutengeneza kuwa Genius.
Kiwango cha Kufikiri. Jambo
la pili unalotakiwa kufanya ni kubadilisha mfumo wako wa kufikiri. Unatakiwa uwaze
zaidi namna ya kuongeza ugenius. Unapoanza kuwaza namna ile utajikuta unapenda
kujifunza zaidi kwa wengine waliotangulia hapo ndipo ugenius wako utajijenga na
kukua. Unapokuwa na uhuru wa kufikiri kisha tena akili yako iko tayari
kufikiria, huo ni msingi imara wa
kujitengeneza kuwa genius.
Kwa maoni yangu kila mtu
anaweza kuwa genius akitaka. Kwanza awe na uhuru au muda wa kufikiria kuhusu kuwa
genius pili awe tayari kuitumia akili yake ili iweze kumpa matokeo makubwa.
Amua leo kuwa genius halafu utaona matokeo makubwa.
0 comments:
Chapisha Maoni