Jana kuna watu wengi wameweza kufanya mambo yao vizuri tu bila ya wewe kuwepo. Kuna siku ambazo hukuweza kwenda kwenye kazi yako au biashara yako na waliopo chini yako waliweza kufanya kazi zao bila ya matatizo.
Mtoto wako au mdogo wako au yeyote ambaye yuko chini ya uangalizi wako kuna wakati ameweza kufanya maamuzi muhimu kwake bila hata ya wewe kuwepo.
Ninachotaka kukuambia hapa ni nini?
Ninachotaka kukuambia hapa ni nini?
Najua umekuwa unajaribu kuwa kiranja wa dunia nzima. Kwamba ili kitu kifanyike vizuri ni lazima wewe uwepo, ukifanye wewe mwenyewe au ukisimamie kwa karibu. Hizi ni hisia ambazo watu wengi wanakuwa nazo na zinawanyima uhuru, kuwachosha na kushindwa kuwaamini wengine.
Unachotakiwa kujua ni kwamba watu wengine pia wanaweza kufanya majukumu yao vizuri bila ya wewe kuwepo moja kwa moja. Muhimu ni wewe kuwaelekeza
vizuri ni kipi wanachopaswa kufanya kisha wape uhuru wa kufanya, bila ya wewe kuwepo moja kwa moja.
Hofu yako ni kwamba watakosea, ndiyo lazima watakosea, lakini ni kupitia makosa yao ndiyo watajifunza zaidi.
Na wanapoanza na makosa madogo ndivyo wanavyoweza kuepuka makosa makubwa. Lakini kama utawazuia kabisa kufanya makosa madogo madogo, watakuja kufanya makosa makubwa ambayo yatawagharimu sana.
Hii ni kwa wote ambao wanasimamia wengine, wameajiri wengine, wazazi na walezi na mtu yeyote ambaye anapenda kudhibiti na kusimamia kila kitu. Huwezi kuwa kiranja wa dunia nzima, utaumia na kuwazuia wengine kukua. Hakikisha watu wanajua wajibu wao kisha wape uhuru. Wanafanya vizuri zaidi wakiwa na uhuru kuliko wakiwa wanasimamiwa kwa karibu sana.
UKWELI NI KWAMBA Inawezekana Umekuwa unajaribu kuwa kiranja wa dunia. Umekuwa unakazana kuhakikisha kila kitu unakifanya wewe mwenyewe au unakisimamia mwenyewe. Lakini hili limekuwa linakuumiza na kukuchosha na pia linawanyima wengine fursa ya kujifunza, kukua na kufanya kwa uhuru. Kuanzia sasa hahakikisha wengine wanayajua majukumu yao vizuri kisha wape uhuru wa kuyafanya wao wenyewe.

CHUKUA HII.
“There is no greater power and support you can give someone than to look them in the eye, and with sincerity/conviction say, 'I believe in you.” ― Ken Poirot
“There is no greater power and support you can give someone than to look them in the eye, and with sincerity/conviction say, 'I believe in you.” ― Ken Poirot
(Hakuna nguvu kubwa na msaada unaoweza kumpa mtu kama kumwangalia machoni kwa uaminifu na ushawishi na kumwambia NINAKUAMINI).
Amini kwamba wengine wanaweza kufanya makubwa bila ya kusimamiwa moja kwa moja na wewe. Wape uhuru wa kufanya kile wanachopenda kufanya.
0 comments:
Chapisha Maoni