Jumamosi, 2 Aprili 2016

Jishughulishe Na Matatizo yako Kwanza!


 
Wakati mwingine Tunapenda sana kushughulika, kuzungumizia, au kutatua matatizo ya wengine. Kila mmoja wetu ana ndoto kubwa ya kutatua matatizo ya dunia, kuibadili dunia, kuifanya dunia kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi. Ila haya yote yanawezekana kama hiki kimoja kitafanyika, kuanza kutatua matatizo yako kwanza. Ni lazima uanze na matatizo yako kwanza, uweze kuyatatua, na baada ya kuyatatua ndiyo unaweza
 
kutatua matatizo ya wengine. Kutatua matatizo yako kwanza kunakupa haya mawili muhimu;

1.Kunakupa uzoefu wa jinsi unavyow
eza kutatua matatizo na hivyo kuweza kuwashirikisha wengine
njia ulizotumia wewe.

2. Kunakupa amani ya moyo, unakuwa na utulivu kwamba tayari matatizo yako yameshatatuliwa.
 
Kujaribu kutatua matatizo ya wengine wakati bado ya kwako yanakusumbua, mawazo yako
hayatakuwa kwenye kile unachofanya na hivyo huwezi kufanya kwa ubora.

 
Anza na matatizo yako mwenyewe, kisha yafanyie kazi matatizo ya wengine na matatizo ya dunia.

UKWELI NI KWAMBA  ili uweze kutatua matatizo ya wengine vizuri, unahitaji kutatua matatizo yako kwanza. Kwa kutatua matatizo yako utakuwa na uzoefu mzuri na pia utapata amani ya moyo na hivyo kuweza kusaidia kwa moyo mmoja.
 
CHUKUA HII
“Every problem is a gift - without problems we would not grow.” ― Anthony Robbins
(Kila tatizo ni zawadi, bila ya matatizo hatuwezi kukua).

 
Tatua matatizo yako kwanza kabla hujatatua ya dunia, utapata uzoefu wa kutatua na pia utapata amani ya moyo.


0 comments: