Hizi ni baadhi tu ya kauli za baadhi ya watu ambao ni wafuasi wakubwa wa kitu kinachoitwa bahati mbaya;
“Alikuwa anavuka barabara, lakini kwa bahati mbaya akagongwa na gari.” “Nimemaliza masomo yangu mwaka jana, lakini kwa bahati mbaya nikafeli.” Kwa bahati mbaya biashara yangu ilisambaratika.” “Kwa bahati mbaya alifukuzwa kazi.” Imetokea kwa bahati mbaya” Nimebata bahati mbaya Mume wangu hanifai hata kidogo.” “Kwa bahati mbaya alijifungua mtoto aliyekufa”. Hebu tujifunze vyanzo vya bahati mbaya na namna ya kuepukana navyo, ili tusijikute kila siku tunalaumu kupatwa na bahati mbaya kumbe makosa ni yetu na kwamba hatukuwa makini katika kuishi kwetu.

1. Uzembe wa Kufikiria
Watu wengi wanaoamini kuwepo kwa matukio ya bahati mbaya katika maisha wanaelezwa na wataalamu kuwa na kasoro katika upeo wa kufikiri vyanzo vya mambo. Inasemwa na watafiti wengi kuwa matukio mabaya yaliyopata kuripotiwa ulimwenguni ni ma
tokeo ya uzembe wa kufikiri na kuamua. Kwa maana hivyo inashauriwa
kuwa mtu anayetaka kuepukana na bahati mbaya lazima awe hai katika
fikra, hasa upataji wa jibu la mapema juu ya nini kitatokea katika kutenda kwake.Watu wengi wanaoamini kuwepo kwa matukio ya bahati mbaya katika maisha wanaelezwa na wataalamu kuwa na kasoro katika upeo wa kufikiri vyanzo vya mambo. Inasemwa na watafiti wengi kuwa matukio mabaya yaliyopata kuripotiwa ulimwenguni ni ma
Inampasa mvuka barabara kwa mfano, ajiuliuze matokeo
ya kuvuka kwake na apate majibu chanya na hasi na ahakiki matokeo hasi
ambayo kwa kawaida ndiyo yenye madhara. Vivyo hivyo kwa dereva
anayeendesha chombo cha moto, msichana anayetaka kuolewa, mfanyabiashara, mfanyakazi, anayefanya mapenzi, anayesoma, wote kwa ujumla wao lazima wawe na majibu ya kwa nini wanataka/ wanafanya hayo, kisha wajadili akilini matokeo mabaya ambayo yapo na kuyatafutie njia ya kuepukana nayo.
2. Kutotumia Uwezo Wote
Mwanadamu natajwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo kuliko wengi wao wanavyodhani. Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuwa asilimia 70 ya watu ulimwenguni, hasa wale wa dunia ya tatu wanaishi chini ya uwezo na vipaji walivyonavyona. Kwa kuzingatia hilo wahanga wengi wa bahati mbaya ni wale ambao hawatumii uwezo wao wote au zaidi ya nusu ya vipaji vyao katika kupambana na matokeo mabaya.

Wanafunzi wengi hawasomi kwa uwezo wao wote,
wataalamu, wanasiasa, viongozi, watendaji hawatumii uwezo wao wote
kufanya kazi na majukumu waliyonayo, matokeo yake wanalipua kazi na
baadaye kuleta matokeo mabaya kisha kuyapa jina la BAHATI MBAYA.
Inasemwa kuwa kila mahali palipo na janga msingi wa kwanza kutazamwa kwa
watu wenye uelewa ni UZEMBE na kutotumika kwa uwezo halisi wa wahusika
katika kukinga matokeo mabaya.
3. Kuamini Viashiria vya Kushindwa
Kuna watu ambao hupatwa na matokeo ya bahati mbaya baada ya kuamini viashiria vya kushindwa na kuacha kujizatiti katika nguvu za ushindi. Kwa mfano timu ya mpira inaweza kufungwa magoli 3 kipindi cha kwanza, matokeo hayo yakiaminiwa na wachezaji yanaweza kunyonya nguvu ya ushindani na kuikaribisha bahati mbaya, kumbe wangepuuza viashiria hivyo vya kushindwa mapema wakaongeza nguvu wangeweza kurudisha na pengine kushinda mchezo.

Vivyo hivyo, tunapokuwa tunafanya jambo fulani, kuna
viashiria vinaweza kujitokeza kututia hofu kwamba tutashindwa,
tunashauriwa kutokata tamaa. Kama
wewe ni muuguzi umemuona mgonjwa wako anashindwa kupumua usipunguze
harakati za kumtibu kwa kuamini viashiria kwamba anakufa muda mfupi
ujao, badala yake zidisha juhudi za kumuokoa. Mfanyabiasha pia ukiona
biashara inayumba usikate tamaa, ongeza bidii kwa kufanya hivyo utakuwa
unapambana na bahati mbaya na kwa mujibu wa wanasaikolojia utakuwa
umenyonya nguvu za mabaya na hivyo kutokukupata.
4. Kuyumba Katika Maamuzi
Kuna watu ambao kwa hakika kabisa wanaweza kuwa wamefikiri vema, wametumia uwezo wao wote, hawakuamini viashiria, lakini wakajikuta wanapatwa na bahati mbaya kwa kuyumba katika maamuzi, hasa wakati wa kuhitimisha jambo fulani.

Kwa mfano mtu anaweza kuwa ametafuta mchumba, akamhakiki kama
nilivyosema, lakini likatokea neno la umbea fulani likamyumbisha na
akajikuta amemwacha mchumba wake na kuchukua mwingine ambaye hakumhakiki
katika fikra. Inashauri kwamba mtu asiyumbe katika maamuzi sahihi
aliyoyathibitisha.
5. Kumbukumbu Mbaya
Katika maisha yetu kuna watu wengi ambao wanasogeza bahati mbaya kwa kujaza kumbukumbu mbaya za matukio hasi kwenye akili zao. Wapo mahodari wa kukumbuka mahali zilipotokea ajali za magari, yaani wakifika hapo tu mioyo inakwenda mbio. Kuna wanaokumbuka rafiki zao waliokufa wakati wanajifungua na wengine wana historia za nani alipatwa na mabaya baada ya kufanya jambo fulani na wengine wanawafahamu kwa majina waliokufa bila kuzaa, yote hayo ni kujitia hofu tupu.

0 comments:
Chapisha Maoni