Habari yako Ndugu na Rafiki yangu mpenzi.
Katika maisha haya tunayoishi, tunakutana na changamoto nyingi sana, wengine hukata tamaa, huishia kulalamika, kulaumu wengine n.k.
Lakini ukweli ni kwamba katika changamoto nyingi tunazokumbana nazo zimebeba majibu yake, na ndani ya majibu hayo kuna fursa nzuri. Hebu pitia kwa ufupi tu kisa hiki cha baba na mwanaye......
Baba mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti chake chini ya mti anasoma gazeti. Pembeni yake alikuwepo mtoto wa miaka 6 ambaye alikuwa akimsonga kwa maana nae alikuwa anataka kuangalia kilichomo ndani ya gazeti.
Baba huyu ili kuondoa usumbufu akaona ni vema achane ukurasa mmoja ili ampatie mwanae. Ukurasa huu ulikuwa na ramani ya dunia, akamuonesha “unaiona hii ramani eh? baba yake akaichana ile ramani vipande vidogo vidogo kama kumi na tano.Akamwambia mwanangu nenda ukavipange hivi vikaratasi mpaka iwe ramani kama ilivyokuwa, ntakupa booonge la zawadi. Hii yote ikiwa ni katika kuondoa usumbufu.
Mtoto akaenda kujifungia baada ya dakika chache akarudi akiwa amevipanga kwa usahihi kabisa. Kwamshangao haaaaaa!! Umewezaje kufanya haraka hivyo? mtoto akajibu nyuma ya vikaratsi hivi ilikuwepo picha ya sura ya mtu hivyo nilivipanga kwa kukufuta sura hiyo.
Unajua maishani suala si kukutana na changamoto bali ni jinsi gani unazichukulia changamoto hizo. Ukikutana na changamoto yoyote tuliza akili na utapata mlango wa kutokea Changamoto nyingi hapa duniani ukigeuza upande wa pili utagundua ni FURSA. Fanya hivyo utashanga mambo yanavyokuwa rahisi kwako.Ila ukiwa kipofu wa kuitazama ile changamoto kwa hisia za itakuwaje utabaki hapo hapo.
Hatupaswi kukata tamaa kwa sababu ya changamoto tunazokutana nazo, bali tunapaswa kuchunguza kwa umakini mkubwa ili kuziona fursa zilizo ndani yake.
0 comments:
Chapisha Maoni