Katika ujauzito, mwili wa mwanamke hubadilika kwa njia nyingi . Matatizo haya yanaweza kumkosesha utulivu. Hata hivyo, mara nyingi huwa ya kawaida. Yanaweza kutokea wakati wowote katika ujauzito.
Hapa, tutajifunza kuhusu baadhi ya matatizo madogo ya ujauzito na kujadili njia za kuwasaidia wanawake kujihisi vyema au angalau waache kuwa na hofu kuyahusu. Pia tutajifunza jinsi ya kutambua ukosefu wa utulivu kwa mwanamke unapoashiria kuwa huenda kukawa na tatizo linalohitaji uchunguzi zaidi na udhibiti, au hata kuwa jambo la hatari linatendeka kwa ujauzito wake.
Mengi ya matatizo haya madogo katika ujauzito yanaweza kupunguzwa kwa elimu bora na matibabu ya mara moja. Pia unapaswa kujua kuhusu baadhi ya tiba zilizo hatari kwa wanawake wajawazito na zinazoweza