Na Peter Mkufya Stewart
Katika makundi makuu ya watu wanaojenga uchumi wa taifa lolote duniani ikiwemo Tanzania yaani Waajiri na Waajiriwa wanaonekana kuishi katika dunia moja na mazingira yanayofanana lakini kila kundi katika matumizi ya muda linasukumwa na malengo tofauri kabisa.
Mwajiri kila kunapokucha muda wake mwingi anawaza na kusukumwa na namna ya kukuza uchumi yaani kuongeza kipato ili aweze kukidhi mahitaji ya wafanyakazi wake, gharama za mtaji na kujijenga zaidi. Hili halimpi usingizi Mwajiri.
Kwa upande mwingine, Mwajiriwa kila kunapokucha anatumia muda wake mwingi kufikiri na kukimbizana na malengo aliyowekewa na Mwajiri ikiwa ni pamoja na kukamilisha vimeo vya kazi vinavyomnyima raha. Kwa hili Mwajiriwa hapati usingizi.
Mwajiri na Mwajiriwa wote wanapewa masaa sawa yaani masaa 24 kwa siku. Tofauti ni malengo na mgawanyo wa matumizi ya masaa hayo kama nilivyo eleza hapa juu.
Huu ni ukuta mkubwa kati ya Mwajiri na Mwajiriwa. Katika hali hii,
Mwajiriwa (mtegemea mshahara) hawezi kuwa mwajiri (Mjasiriamali) mpaka atakapo amua kuruka ukuta huu. Pasipo kuruka ukuta huu usijidanganye kuwa ipo siku utajikuta umekuwa Mwajiri baadala Mwajiriwa!. Huwezi kupanda spinachi utegemee kuvuna mchicha.
Je ungependa kujua namna ya kuruka ukuta huu salama?.
Je ungependa kuhama kutoka kwenye matumizi ya muda unaojikita katika kukimbizana na kukamilisha vimeo vya kazi na malengo uliyopangiwa kwa muda husika, nakuhamia kundi linalo pambana kuongeza kipato na kiu ya namna ya kupata mapato zaidi badala ya hofu ya majukumu uliyokabidhiwa na mwajiri?.
Umejibu, ndio!. Basi endelea kusoma sehemu inayofuata, ili ikujengee uwezo wa kutumia mbinu hizi.
Zawadi Kwa Watanzania
Zawadi Kwa Watanzania
0 comments:
Chapisha Maoni