Jumamosi, 6 Februari 2016

KUKUZA UCHUMI.

                                                              PETER MKUFYA STEWART
Swala la kufanikiwa kimapato (income) si swala la kuwa na elimu kibwa au kufanya kazi miaka mingi. Fikra zako ndizo zinazokupa nguvu na matendo (Actions) ya kiwango cha mapato unayotaka. Wapo watu fikra zao ni kuwa hawawezi kuja kupata milioni 100. Tena ukitaka wakucheke wape mpango wakupata bilioni 1. Wanaona hawastahili. Wamesha amini hawawezi. Matendo yao, kauli zao, marafiki, mtandao wao (Network) n.k, vime ambatana na hisia kuwa hawawezi kujenga
kipato hicho. Jambo ambalo sikweli. Katika hali ya kawaida, spidi ya kukuza kipato si ya mwanga (light) ni ya mfumo wa matone (drops). Hebu tuangalie kanuni ya 'kumi-kumi' inavyoweza kukusaidia kubadili fikra na kuanza safari yako kufikia kipato cha juu. Kanuni hii inaanza na shilingi 100, kiasi ambacho kila mtu amewahi kukipata. Kama umeshawahi kupata shilingi 100, unauwezo wa kupata shilingi elfu 1 na kuendelea. Angalia kanuni ya kumi-kumi;
Tsh 100 zikiwa 10 ni elfu 1.
Elfu 1 zikiwa 10 ni elfu 10.
Elfu 10 zikiwa 10 ni laki 1. Laki 1 zikiwa 10 ni milioni 1.
Milioni 1 zikiwa 10 ni milioni 10.
Milioni 10 zikiwa 10 ni milioni 100.
Milioni 100 zikiwa kumi ni bilioni 1!.
Nirahisi kusema tatizo lako ni kuwa ukipata fedha, baada ya dakika chache zinakwenda kwenye matumizi. Tunaweza kutumia tabia ya bahari (Ocean) kudhibiti hali hiyo ( Tabia ya bahari imeelezwa). Japo bahari ina staajabisha kwa maji mengi ukweli ni kuwa inategemea mito na vijito kudumisha uwingi wa maji yake. Katika safari ya kukuza kipato, miongoni mwa mbinu rahisi ya kupata mtaji ni ile ya 'Fikra Wezekana' (Possibility Thinking) ya mmarekani aitwaye Dr. Robert Schuller, aliyoieleza kwenye kitabu chake kiitwacho "Tough Times Never Last But Tough People Do" akiwa ana maana kuwa "Nyakati za Dhiki Hazidumu ila Mtu Imara Atadumu" (Mbini hii imeelezewa). Shauku ya kuwa na bilioni 1, hujenga fikra za kuwa na bilioni 1. Fikra za kuwa na bilioni 1, hujenga matendo (Actions) ya kuwa na bilioni 1. Matendo hayo huleta matokeo (results) ya bilioni 1. Ndio maana, kama umeshawahi kupata shilingi 100 basi uwezo wakupata bilioni 1 unao. Ndio, unao. Anza leo kujenga  kipato chako na taifa lako kwa ujumla. Safari hii ya kuelekea kwenye bilioni 1 si rahisi sana ninavyoijua. Utajikwaa, usihofu. Utaanguka, simama.  Hatimaye, utafika. Nakutakia safari njema. Tukutane kwenye bilioni 1.
Zawadi Kwa Watanzania by Peter Mkufya.

0 comments: