Ijumaa, 5 Agosti 2016

MAMBO 6 UNAYOPASWA KUACHANA NAYO LEO ILI USIFE MASKINI



Watu wengi wanakufa masikini na wanashindwa kufikia mafanikio yao bila wao kujua tatizo ni nini,imekuwa kama ugonjwa watu wengi kuendelea kulalamikia serikali au wazazi wao kuwa wao hawafanikiwi wao ndio sababu,na wengine wamekuwa wakikata tamaa kabisa ya mafanikio yao bila wao kujua nini kinachokwamisha maisha yao kuwa bora.

Leo tutajifunza pamoja vizuwizi vya mafanikio yako ambapo kama utavifanyia kazi basi utaanza kushuhudia mafanikio yako,ni muujiza mkubwa sana utatokea kwako hakuna aliezaliwa kuwa masikini rafiki.soma kwa makini.

1.UOGA ( _Fear_)
Hichi ni kikwazo kikubwa sana kwa watu wengi katika kuyafikia mafanikio yao, watu wengi wamekuwa masikini na wengine kufa masikini kwasababu ya uoga, uoga wa kukataliwa na uoga wa kushindwa, kama unataka kufanikiwa katika kila kitu kwenye maisha yako usiogope kuomba au kusema chochote mbele ya watu eti kwa kuogopa kukataliwa! Rafiki usiusemee moyo wa
mwenzio usiogope!! lakini pia usiogope kushindwa yani mtu anataka kufanyabiashara lakini kitu cha kwanza anawaza ni kushindwa anaamini kuwa yeye hawezi na akianzisha atafeli.

Rafiki acha uoga kwani huo ndio umasikin wako, ushinde uoga ufanikiwe.

2. KUKOSA MSUKUMO ( _Lack of aggressiveness_ )
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika maisha yao kwa sababu ya kukosa msukumo binafsi. Rafiki yangu, hakuna mtu yeyote ambae atakaa chini na kupanga maisha yako au kuna mtu ataacha shughuli zake kwaajili ya kupigania maisha yako, wewe ndiye unayejua ugumu na uchungu wa maisha yako!! Amka sasa kuwa na msukumo kutoka moyoni mwako wa kushinda, usisubiri mtu fulani aje akuambie nenda kazini au fanyabiashara. Wewe mwenyewe kaa chini jitume utafanikiwa.

3.UJASIRI NA KUJIAMIN ( _Courage and confidence_)
Hapa ndipo balaa!! Watu wengi sana wanakosa kujiamini wenyewe. Rafiki yangu hebu jiamini kuwa wewe unaweza. Amini kuwa ndani yako kuna mtu mkubwa saana na anayeweza kufanya vitu vikubwa pia, Acha kusikiliza watu wengine wanasema nini kuhusu wewe, Usikilize moyo wako unasema nini kuhusu wewe, Usikubali kushindwa!! Thubutu kwa kila jambo unaloambiwa lenye mafanikio na usiamini kuwa wewe huwezi unaweza. Na zaidi ya yote usikubali kuogopeshwa na watu wengine. Wapo watu watakuvunja moyo na kukuambia eti ndoto yako ni kubwa sana na kwamba hutaweza kuifikia. Wapuuzie watu wa namna hiyo na utumie maneno yao kama kichocheo cha wewe kutafuta kufanikiwa zaidi na zaidi.

4.KUKOSA LENGO MAALUMU ( _Lack of purpose driven goals_)
Rafiki malengo yako nini? Lengo ni ndoto zenye mipaka. Kuna Malengo ya Muda Mfupi, Malengo ya Muda wa Kati na Malengo ya muda mrefu. Jewewe malengo yako ni yapi? 

Rafiki yangu lazima ufahamu kuwa, huwezi kufanikiwa katika maisha yako kama huna malengo ya maisha yako!! Kama huna malengo, basi panga leo. Yaandike malengo yako. Mtu asiye na malengo ni sawa na mtu ambae anaenda stendi kupanda gari lakini hajui anaenda wapi, atapanda gari gani na atashukia wapi!!! Huyu mtu hatofika popote bali atazunguuka na gari hadi usiku gari linapokwenda kupaki basi litamshusha popote. Tambua Malengo yako na kamwe usiwe mtu wa BORA LIENDE.

5.KUTOKUJITUMA ( _Lack of commitment_)
Kujitoa limekuwa tatizo kwa watu wengi sana, na linawakwamisha watu wengi sana kuyafikia mafanikio yao.
Mara nyingi watu wanafanya mambo yao kwa mazowea, uzembe na uvivu uliokithiri. Kamwe huwezi kufanikiwa kwa kufanya kitu kile kile kwa njia ileile, juhudi na mbinu zilezile na utegemee kufanikiwa!! 

Rafiki yangu ili ufanikiwe nilazima ujitume kikamilifu kwa kujitoa na kuwekeza nguvu, muda na maarifa yako kwenye shughuli zako, iwe ni kazi ya kuajiriwa, biashara nk. ndipo utakapoona mafanikio yakija. Acha uvivu, uzembe na kufanya mambo kwa mazowea, Jitoe, Jitume, Pambana na utafanikiwa.

6.KULINDA MUDA ( _Time management_ )
Watu wengi wanaposikia muda ni mali huwa hawaamini leo nataka ujue uhusiano uliopo baina ya muda wako na umasikini wako au utajiri wako.

Unatumiaje muda wako ambao unatoka kazini? unatumiaje muda wako ambao unatocha chuo? wewe mama wa nyumbani unatumiaje muda wako ambao unakuwa hauna kazi nyumbani? hapa ndipo kasheshe na umasikini wa watu ulipo.

Kila sekunde na saa inayopita lazima uhakikishe unafanya kitu ambacho chenye manufaa kwenye maisha yako,mfano ukitumia masaa mawili unajifunza kitu chenye mafanikio kwenye maisha yako basi unayavuta mafanikio yako masaa mawili kama mafanikio yako yalikuwa uyafikie kwa siku mbili na masaa mawili basi utakuwa umebakisha siku mbili.

Kama unatumia muda wako kuangalia TV, kupiga umbea, kupiga story zisizokuwa na maana ukifanya hivyo masaa mawili kwa siku ndani ya mwaka utakuwa umepoteza zaidi ya miezi 4, basi hiyo miezi minne ndio umesogeza mbele mafanikio yako. Kwaiyo kama ungetakiwa ufanikiwe kwa miaka miwili basi utafanikiwa kwa miaka miwili na miezi minne.

Sasa watanzania wengi huwa wanapoteza zaidi ya miezi 9 kila mwaka ndani ya miaka 15 tayari ameshasogeza mbele mafanikio yao kwa zaidi ya miaka kumi.kwa hiyo ukichukuwa miaka kumi ya kutafuta maisha na ile miaka kumi aliopoteza ni miaka 20.

Kwa mfano ameanzakutafuta maisha na akiwa na miaka 30-40 miaka ya kufikia mafanikio yake itakua 50 na maisha now ni mafupi hayafiki huko na kipindi anaendelea kutafuta anapoteza tena masaa kadhaa.lazima ufe masikini.amka sasa mtanzania acha kutumia muda wako vibaya kwani muda wako unaoupoteza sasa utakugharimu.
MUDA NI MALI UKIPUUZA HILO UTAKUFA MASIKINI.ACHA KULALAMIKA CHUKUA HATUA.
 
ALL THE BEST

0 comments: