1. Hauwezi kumkemea huyo unayejipendekeza kwake hata kama anakosea.
2. Unakuwa Mtumwa kwa huyo unayejipendekeza kwake.
3. Unaifanya akili yako ishindwe kuzalisha matunda maana Unakuwa Tegemezi kwa huyo unayejipendekeza kwake.
4. Utajikuta unakosana NA watu hasa wakimkosoa huyo unayejipendekeza kwake. Maana huntokubali akosolewe mbele yako.
5.Inakufanya kuwa mnafiki ,Maana hata wewe kwenye uvungu wa moyo wako kuna vitu unaviona havipo sawa lakini "UNAMEZEA TU " Kulinda kufukuzwa.
6. Inakuharibu kisaikolojia ,hasa pale ambapo Hautapata kile Ulichokitegemea kwa Huyo unayejipendekeza kwake.
7.Inakufanya Uyanyonge MAONO uliyonayo kwa mikono yako mwenyewe, maana Muda mwingi unatafuta Jinsi ya kumpendeza Huyo unayejipendekeza kwake. Badala ya kuwekeza Muda wako kwenye MAONO Binafsi.
8.Kunakufanya Huyo Unayejipendekeza kwake awe
"MUNGU MTU " ,Hivyo unajikuta unamsujudia kwa kila jambo.
9. Hauwezi kufanya MAAMUZI Binafsi ni hadi huyo unayejipendekeza kwake akuamilulie, akikataa ndiyo basi tena.
10.Utagombana NA watu mara kwa mara, maana kila atakayejionyesha kuwa karibu NA huyo unayejipendekeza kwake, Utampiga mawe maana unafikiri, anaichukua nafasi yako.
11. Inakufanya uthamani wako Ushuke kabisa NA kudharaulika , Maana unaishi kwa kumtegemea Mwanadamu mwenzako bila yeye haukai mjini.
12. mungu wako anakuwa ni huyo UNAYEJIPENDEKEZA KWAKE.
13.Hauwi Mwanaume halisi /Mwanamke halisi, Maana walio Halisi wanayo misimamao Binafsi wala hawayumbishi kama uliyo wewe kwa huyo, UNAYEJIPENDEKEZA KWAKE Maana umekuwa ."BENDERA FUATA UPEPO "
USHAURI WA BURE
1.Acha Kujipendekeza.
2. Wewe ambaye MTU/WATU WanajipendekeA kwako. ...kwa kuwa sasa unaabudiwa (kimungu mtu wewe ),Mungu atakushusha hadi kuzimu.
3.HERI KUJIPENDEKEZA KWA MUNGU MAANA ANAKUWA NI MUNGU WAKO NA UNAKUWA MTUMWA WAKE NA ATAKUAMULIA MAAMUZI YAKO.
0 comments:
Chapisha Maoni