Kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kuniuliza, “unapataga wapi ujasiri wa kuongea mbele za watu”? Mbona mimi huwa siwezi?.
Nilimjibu kwa kifupi tu kuwa “mimi huwa siwezi kuongea mbele za watu ikiwa sijui cha kuongea au sina sababu ya kuongea. Mara nyingi huwa niko kimya mpaka nipate sababu ya kuongea na niwe ninajua ninachotakiwa kuongea”.
Akaniuliza tena, “sasa huwa unapata wapi cha kuongea”?. Nilimjibu “mpaka nipate sababu ya kuongea ndipo nipate cha kuongea”.
Akauliza swali la mwisho akasema “wakati mwingine huwa ninasababu ya kuongea lakini siwezi kabisa kuongea tatizo nini”? Nikamjibu kuwa “tatizo linaweza kuwa ni moja ya sababu zifuatazo au zote kwa pamoja”
.
Sababu
zinazokufanya ushindwe kuongea mbele ya watu wengi na jinsi ya kukabiliana nazo.
Sababu ya kwanza: Hujui
protocol ( mpagilio wa namna ya kuanza hadi kumaliza)
Kutojua mahali pa kuanzia kuongea mbele ya watu ni
sababu
kubwa ya watu wengi kushindwa kuongea mbele ya watu wengi.
Mfano ukiwa kwenye vikao vya kawaida huwa kunautaratibu wake uanze na nani kumtaja kama kuna watu wenye cheo unatakiwa uanze kuwataja, namna ya kutoa salamu kwa watu hao, ukaribisho unaoendana na mazingira ya kikao au mkutano huo na jinsi ya kuunganisha tukio moja na jingine. Kutokufahamu mpagilio huo ukipewa nafasi ya kuongea mbele ya watu wengi miguu itaishiwa nguvu kwa woga. Lakini kwa mtu anayefahamu hizo protocol atatiririka mwanzo mpaka mwisho.

Nini cha kifanyike?
Unatakiwa ujifunze namna ya kufuata protocol vizuri,
jaribu kuulizia watu walioko karibu yako wakuelekeze namna ya kunzingatia hizo protocol,yaani
namna ya kutoa salamu, namna ya ukaribisho na kila jambo linalohusu protocol. Ukifanya
hivyo utakuwa ukipewa nafasi ya kuongea mbele ya watu wengi utakuwa unatiririka
mwanzo hadi mwisho.
Sababu ya pili: Unamisamiati
michache.
Kuwa na misamiati michache kinywani mwako kuna punguza
ujasiri wa kuongea mbele ya watu wengi.
Mfano umeenda kwenye ibada halafu unateuliwa utoe mahubiri halafu hujui maandiko, unafikiri kitu gani kitatokea? Lakini ukimpa nafasi hiyo mtu mwenye ufahamu wa maandiko (ana misamiati mingi) atatiririka mpaka muda mtaona hautoshi maana kila neon atakalokuwa anatamka litakuwa linafuatiwa na maneno mia moja mengine nyuma yake.
Hata utashangaa anakuwa anashindwa aanze na lipi maana ana “alternative” ya maneno chungu nzima. Kuwa na msamiati mwingi kwenye ajenda unayozungumzia kuna kufanya uwe na ujasiri mwingi wa kuongea.

Nini kifanyike?
Kama una fursa ya kupewa nafasi ya kuongea mbele ya watu
wengi mara kwa mara, jitahidi sana uwe na msamiati mwingi.
Ikiwa ni kwenye sehemu za ibada jitahidi usome sana maandiko halafu utashangaa unabobea kuongea mbele ya watu wengi kwa sababu unakuwa umejaa msamiati mwingi. Vivyo hivyo kwenye sehemu zingine mfano mzuri bungeni, wabunge wenye msamiati mwingi ( wanaupata kwa kupitia kusoma sana ) utawaona mara kwa mara wakichangia tena kwa kutoa hoja nzito. Lakini wale wenye misamiati michache kazi yao ama kusinzia au kupiga makofi.

Sababu ya tatu: Unajidharau
au unajiona una elimu ndogo kuliko wao.
Kujidharau ni kosa kubwa au ni sababu kubwa ya watu
wengi kushindwa kuongea mbele ya watu.
Mtu anasimama kuongea mbele ya watu labda tuseme anaongea na wanachuo halafu yeye yuko kidato cha nne. mtu huyo kama ana tabia hii ya kujidharau hataweza kuongea kwa ujasiri mbele ya watu hao. Ataongea maneno mawili tu halafu anakaa kimya kwa kuogopa kuonekena hajui.

Siku moja wakati naperuzi facebook kuna mtu mmoja aliweka picha ya paka ( nyau) anajiangalia kwenye kioo. Chakushangaza kwenye picha hiyo paka hajioni kama paka ila anajiona kama simba.
Ndivyo unatakiwa kuwa hata wewe kwenye kila jambo unalolifanya unatakiwa kujiona sio kama paka tena ila unatakiwa kujiona kama simba. Hii iweke kichwani mwako siku zote za maisha yako. Ukifanya hivyo hautajidharau kamwe bali utajiona ni mkubwa, saa nyingine kuliko hata wao japo wanakuzidi mambo fulani fulani hivi.
Hilo utaliweza tu ikiwa unamalengo ya kufika mbali zaidi kwenye jambo unalolifanya. Utakuwa unajiona uko juu kuliko wote kwa muda sio mrefu ujao, sasa ukiwa unajiona uko juu kuliko wao utapata ujasiri sio wa kujidharau tena bali wa kujiona wewe ni shujaa.
Sababu ya nne: Unaogopa
utachekwa au utasemwa vibaya.
Kuna mtu anashindwa kuongea mbele ya watu kwa sababu
watu fulani watamcheka.
Sio kwamba anajiona mdogo au anajidharau hapana lakini anaogopa labda mke wake, au mume wake au rafiki zake au watu wa upende fulani watamcheka. Hii hutokea mara nyingi mfano mtu ameenda kwenye chama fulani au dini fulani tofauti na yake, japokuwa anamsamiati wa kutosha na anajua protocol zote lakini anashindwa kuongea kwa sababu watu fulani watacheka au kumsema vibaya.

Unapotaka kusema au kuongea mambo yako mbele ya watu
usitake kujiuliza uliza watasemaje, wewe poromosha maneno yako watakao kucheka
au kukudharau shauri yao wewe umeshatwanga ya kwako.
Sababu ya tano: Kujihisi
mkosefu kwa sababu ulifanya kosa fulani na ukawa unahisi watu wanafahamu kosa
ulilolifanya.
Mtu akifanya kosa fulani wakati mwingine dhamiri yake huwa inamshitaki. Kwahiyo akipewa nafasi ya
kuongea mbele ya watu, ujasiri wote unamwishia kwa sababu ya fikira au dhamiri
yake kumshaitaki mara kwa mara.
Nini kifanyike?
Ikiwa sababu ndio hiyo inayokufanya ushindwe kuongea
mbele ya watu, basi unatakiwa kutafuta ushauri nasaha (counseling) ili ufute fikira hizo. Kuna njia
nyingi za kupata ushauri nasaha mfano unaweza ukasoma vitabu vya Mungu, au
unaweza kumtafuta mashauri akakupa counseling.
Mtu asipokuwa amefanya maandalizi ya kutosha ni vigumu sana kuongea mbele ya watu wengi. Unaweza ukawa wewe ni mkuu wa kitengo fulani halafu kuna taarifa unatakiwa uitolee hotuba mbele ya watu na saa nyingine umeandaa risala au hotuba lakini hujaiandaa wewe umeandaliwa na wasaidizi wako. Utaona jinsi ilivyo tabu kuongea juu ya ajenda hiyo ikiwa huna maandalizi ya kutosha.
Nini kifanyike?
Kabla ya kuongea mbele
ya watu wengi, jiandae kwanza. Unatakiwa ujiandae siku zote (be aware) ikiwa
itatokea umekaribishwa kuongea mbele ya watu hao angalau uwe umeshajiandaa kwa
kiasi fulani.
Sababu ya saba: Kujihisi umepungukiwa.
Kupungukiwa kuna
maana nyingi lakini mimi nazungumzia
kupungukiwa kwa baadhi ya haiba ya binadamu, mfano mtu anaweza akawa na sauti
kubwa sana wakati yeye ni mwanamke au mwanaume anaweza kuwa na sauti ya kike au
mtu anaweza kuwa ana ulemavu wa viungo vya mwili nk. Katika mazingira hayo mtu
huyo hujinyanyapaa yeye mwenyewe na hata akipewa nafasi ya kuongea mbele ya
watu hawezi.
Nini kifanyike?
Usijinyanyase wewe
mwenyewe jikubali jinsi ulivyo na ujione unaupendeleo mkubwa kuwa jinsi ulivyo.
0 comments:
Chapisha Maoni