Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi, Leonard Mwipugi
(29) amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.
Taarifa zilizotolewa na Mratibu wa Elimu Kata ya Mtenga, Hebron Mwafungo
zimeeleza kuwa mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja
nyumbani kwake muda wa saa sita mchana leo Jumamosi.
Amesema kuwa mwalimu huyo alikwenda kazini kwake na saa 5 asubuhi
alirejea nyumbani na hakumkuta mkewe na baada ya muda walipata taarifa
kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani
kwake.
Amesema kuwa mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake nyumbani hapo na
alipofika alimtuma mdogo wake mbali kidogo ya nyumba hiyo na baada ya
kurudi aliona damu na baada ya kuchungulia chumbani alikuta kaka yake
amefariki dunia kwa kujichinja koromeo na kutoa taarifa kwenye uongozi
wa kijiji hicho.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni