Magonjwa ya zinaa ni magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya
kujamiiyana (sexually transmitted diseases),inayosababishwa na
bakteria,virus au fungus wanaopenda ishi sehemu ya maji maji au unyevu
unyevu katika mwili ,kama mdomoni,kooni,sehemu za siri au sehemu ya
hajakubwa.

Iwapo mtu atakutana kimwili na mtu mwenye maambukizi hapo ni rahisi
kuambukizwa. Magonjwa ya zinaa yanampata mwanamke na mwanaume pia kwa
njia ya mdomo,uuke au uume.
Magonjwa ya zinaa yapo ya aina tofauti kuna
-
Kaswende
-
Kisonono
-
Gonorea
-
Ukimwi
-
Klamidia
-
Malenge lenge sehemu za siri
-
Dutu za sehemu ya siri
Magonjwa ya zinaa ni hatari kwa afya, mama mjamzito akipata ugonjwa wa zinaa atapata dalili tofauti tofauti kama zifuatazo
-
Kuvimba sehemu za siri
-
Maumivu makali pindi ufanyapo mapenzi au wakati wa kukojoa
-
Kupata homa
-
Kutokwa vijipele ukeni vinaweza kuuma au visiume
-
Kupungua uzito
-
Maumivu ya mgongo
-
Kutokwa majasho kwa wingi nyakati za usiku
-
Kutokwa maji maji ukeni yenye harufu au isio na harufu
-
Kutokwa damu au usaha ukeni
-
Kuwashwa sana
-
Uke kubadili rangi
Madhara ya magonjwa ya zinaa kwa mama na mtoto
-
Mtoto anaweza kupata upofu
-
Uziwi-kushindwa mtoto kusikia
-
Mwanamke au mwanamme anaweza kuja kushindwa kuzaa sababu ugonjwa utaenda kuadhiri sehemu za uzazi
-
Kuziba mirija ya uzazi
-
Kifo
-
Ulemavu kwa mtoto
-
Mtu kupoteza kinga ya mwili kuwa dhoofu,kuumwa mara kwa mara.
Tiba
Magonjwa ya zinaa yanatibika iwapo yatatibiwa mapema isipo kuwa
ukimwi peke yake hauna tiba, Kitu cha msingi ni kuwa baada ya kuona dalili zilizoainishwa hapa au zaidi basi wahi kupata ushauri na tiba rasmi hospitalini. mambukizi mengine mama mjamzito atatibiwa
kwa kupewa antibiotic, mtoto iwapo ataadhirika kipindi mama yake
anamimba baada ya kuzaliwa atawekwa dawa machoni ya kusafisha na
kutibu.

MTOTO ALIEPATA MAAMBUKIZI KUTOKWA KWA MAMA ,KAWEKEWA DAWA MACHONI
Iwapo mama amegundulika anamaambukizi na muda wa kijifungua
umekaribia itabidi azalishwe kwa c-section ( operation)ili kumwepusha
mtoto kupata maambukizi.
U.T.I / fungus ni magongwa ya infection nayo yanaweza mpata mama ila
yenyewe hupati kwa njia ya kujamiiana haya yanatokana na virus na
bakteria pia ambao unaweza watoa vyoo vya public au nyumbani iwapo mkiwa
hamsafishi vyoo vizuri na kutumia maji safi ya kujitawazia.

Vyoo vya public,au vya kushare na familia kubwa ni hatari sana kwa mama mjamzito
Hivyo ni vizuri mama mjamzito ukahisi muwasho kwa siku 2-3,maji maji
kutoka ukeni usiyo yaelewa ,kutokwa kijipele wahi hospital wakutibu
kwani nayo ni hatari kwa afya yako na mtoto inaweza sababisha
miscarriage ,tiba utapewa dawa kama ya kupaka ,sindano au kunywa kati ya
hizo.
Baada ya kutumia dawa ya infections,mtu anaweza tumia njia kwa kutoa sumu ya ugonjwa zaidi kwa kutumia vitu asilia kwa kula
-
Kitunguu thomu punje 2 mara 3 kwa siku
-
Kula parachichi
-
Kunywa yoghurt glass 2 kwa siku
Ushauri
Mama unatakiwa kuwa mkweli na muwazi kwa mpenzio ili msilete
ugonjwa wa zinaa na maambukizi yatakayo kuja waadhiri nyie na
mtoto,iwapo mmoja wenu sio mwaminifu mtumie condom.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni